VERONICA MGETA AHIMIZA MSHIKAMANO WA KITAIFA

GEORGE MARATO TV
0


Alieyekua mgombea ubunge wa jimbo la Ilemela Veronica Calist Mgeta katika hutuba yake mbele ya wandishi wa habari amesema kufuatia uungwaji mkono alioupata wakati wa uchaguzi mkuu oktoba 29 Jimbo la Ilemela ni dhahiri kuwa anadeni kubwa kwa wanachi.

“Imani yangu kwa wapiga kura ni kubwa namna mlivyojitokeza hakika ungwaji mkono huu sikua nautegemea hivi mmenipa heshima kubwa maishani mwangu najiona mwenye deni sina cha kuwalipa ila mungu pekee ndie anaweza kuwatosheleza alisema mgeta”

Mgeta amesema kampeni zilizofanyika kata 19 za jimbo la ilemela zimeshuhudiwa  na wananchi  waliojitokeza kwa wingi katika mikutano yetu ya kampeni ili kutusikiliza sera mikakati ya kuwaleta maendeleo wananchi endapo CHAUMMA ingeshinda .

Veronica alisema shukrani pekee hazitoshi ila ataendelea kushirikiana na wananchi wa jimbo hilo katika kuyafikia maendeleo endelevu na kujenga uchumi wa jamii ya wana Ilemela wote kwa kuzingatia misingi ya utu na uzalendo.

Aidha Veronica Mgeta amesema Uchaguzi sasa umekwisha nishukuru wadau wote mlionipigania katika kinyang’anyiro hicho kwa hali na mali zenu ambapo bila nyie nisingeweza kufikia mafanikio niliyoyapata hakika kura zenu ni chachu ya mandalizi ya kupigania demokrasia ya kweli katika uchaguzi unaofata.

Pia amewataka wananchi wa jimbo la ilemela kuendelea kushirikiana baada ya kumalizika kwa Uchaguzi Mkuu wa oktoba 29 mwaka huu ambao ulisimamiwa na Tume huru ya Taifa ya uchaguzi INEC.

Tumefanikiwa kutokana timu imara ya kampeni ambayo ilipambana kuhakisha mimi Veronica Calist Mgeta nafikia malengo ya kuwafikia wananchi wa jimbo zima ambapo changamoto zote zilifanyiwa kazi kwa kushirikiana na uongozi wa chama changu.

Chama cha ukombozi wa umma(CHAUMMA)kimenipa imani kubwa kupeperusha bendela katika uchaguzi uliopita ni dhahili kuwa imani niliyopewa yapaswa kulindwa ili kuimarisha demokrasia imara.

 Niseme uchaguzi umekwisha kama taifa tunapaswa kuimarisha mifumo ya chaguzi zetu ili kupatikana kwa viongozi wanawajibika kwa jamii ya watanzania kuliko ilivyo sasa alisema mgeta.

Mgeta anasema kuwepo kwa uchaguzi huru na wa haki unaozingatia misingi utaondoa malalamiko kwa wadau wa uchaguzi ambao wamekua wahanga wa wizi wa kura na kusabisha kuvuruga amani katika vituo vya kupigia kura.

Licha ya kuwepo kwa changamoto mbalimbali zilizojitokeza viongozi wangu wa chama, timu yangu ya kampeni,wananchi, wadau mlinishika mkono mpaka kukamilika kwa upigaji wa kura kuwa wananchi wa jimbo la ilemela mmenipa mwanga kubwa nami nitaendela kuwa pamoja nanyi kulijenga jimbo letu lifikie mafanikio makubwa ya  kuwahudumia wananchi.      

 

 

 

 


 

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top