Skip to main content

Posts

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Viwango vya Udumavu na Ukondevu Vimepungua Nchini-Majaliwa

_Asema Serikali kuwa lishe ni nguzo ya maendeleo ya rasilimali watu, uchumi na jamii_ _Asema kiwango cha uzito uliozidi na uzito kupita kiasi hasa wanawake wa umri wa kuzaa kimeongezeka_ WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amesema kuwa kiwango cha udumavu miongoni mwa watoto walio chini ya umri wa miaka mitano nchini kimeshuka kutoka asilimia 48 mwaka 1992 hadi asilimia 30 mwaka 2022.  Ameongeza kuwa, kiwango cha ukondefu miongoni mwa watoto walio chini ya miaka mitano kimepungua kutoka asilimia 5 mwaka 1992 hadi asilimia 3.2 mwaka 2022. Amesema hayo leo Jumanne (Septemba 30, 2025) wakati alipofunga mkutano wa 11 wa wadau wa lishe nchini, uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa APC uliopo Bunju Jijini Dar es salaam. Amesema kuwa Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan inatambua kuwa lishe si suala la kiafya pekee, bali ni nguzo ya maendeleo ya rasilimali watu, uchumi na jamii. “Dhamira ya Serikali ni kuhakikisha kila Mtanzania anakuwa na chakula cha kutosh...

Dkt.Nchimbi Aendelea Kusaka Kura za Ushindi wa Kishindo za Dkt.Samia Jijini Dar

Mgombea mwenza wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Emmanuel John Nchimbi akiwahutubia Wananchi kwenye mkutano wake wa hadhara  wa kampeni,uliofanyika leo Septemba 30,2025 katika uwanja wa Kampala-Gongolamboto,Jimbo la Ukonga wilaya ya ilala,jijini Dar es Salaam.  Akiwa katika viunga vya Kampala-Ukonga,Dkt.Nchimbi amewahutubia Wananchi huku akinadi Sera na Ilani ya chama hicho ya 2025-2030 yenye kulenga kuimarisha na kupeleka maendeleo kwa Wananchi.  Aidha, baada ya kuhutubia Wananchi,Dkt.Nchimbi pia alipata nafasi ya kuwanadi baadhi ya wagombea Ubunge wa mkoa huo akiwemo mgombea Ubunge wa jimbo la Ukonga,Ndugu Jerry William Silaa, mgombea Ubunge wa jimbo la Kivule Ndugu Dougras Didas Masaburi na Madiwani. Dkt.Nchimbi ni Mgombea mwenza wa Dkt Samia Suluhu Hassan katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 29, 2025 wakipeperusha bendera ya  Chama   Cha Mapinduzi (CCM), ambapo mkoa wa Dar es Salaam u...

Celebrating Tanzanian Beauty: Miss Tourism Tanzania National Finale on Independence Eve

By Prosper Makene, Senior Journalist Dar es Salaam. The Africa Tourism Promotion Centre (ATPC) and The Miss Tourism Tanzania Beauty Pageants Company Limited today jointly announced a historic alignment that positions the nation's premier beauty and culture showcase, the Miss Tourism Tanzania National Finale, as an annual centerpiece of national pride. The pinnacle event will now be held, every year, on December 8th, the celebratory eve of the United Republic of Tanzania’s Independence Day Anniversary. For 2025, this date holds even deeper significance: it will mark the 10th Anniversary of the Miss Tourism Tanzania National Finale and the launch of the pageant’s transformed system, promising an unprecedented fusion of cultural celebration, sustainable tourism advocacy, and female empowerment. The Unveiling: A Strategic Date for a National Crown "Choosing December 8th is more than a strategic date; it's a statement," says Erasto Gideon, President of the Africa Tourism P...

Fainali ya Kitaifa ya Miss Tourism Tanzania Enzi Mpya Katika mkesha wa Siku ya Uhuru

Na Prosper Makene Kituo cha Kukuza Utalii Afrika (ATPC) na asasi ya Miss Tourism Tanzania Beauty Pageants Limited leo vimethibitisha rasmi ushirikiano wa kihistoria ambao unaziweka Fainali za Kitaifa ya Miss Tourism Tanzania, kama kiini cha kila mwaka cha fahari ya kitaifa na urembo wa kitalii na kitamaduni. Tukio hili kubwa zaidi la urembo wa kitalii na kitamaduni, sasa litafanyika kila mwaka, tarehe 8 Desemba, ikiwa ni mkesha (hawa) wa Siku ya Maadhimisho ya Uhuru wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kwa mwaka 2025, tarehe hii ina maana kubwa zaidi: itaashiria Miaka 10 ya Fainali ya Kitaifa ya Miss Tourism Tanzania na uzinduzi wa Mfumo Ulioboreshwa wa mashindano hayo, ukitengeneza kiini cha muunganiko wa kipekee wa sherehe za kitamaduni, utalii endelevu, na uwezeshaji wa wanawake. Fainali za Taifa: Tarehe ya Kimkakati kwa Taji la Kitaifa. "Kuchagua tarehe 8 Desemba ni zaidi ya tarehe ya kimkakati; ni tamko," anasema Erasto Gideon, Rais wa Kituo cha Kukuza Utalii Afrika (ATPC...