Dkt.Nchimbi Aendelea Kusaka Kura za Ushindi wa Kishindo za Dkt.Samia Jijini Dar

GEORGE MARATO TV
0


Mgombea mwenza wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Emmanuel John Nchimbi akiwahutubia Wananchi kwenye mkutano wake wa hadhara  wa kampeni,uliofanyika leo Septemba 30,2025 katika uwanja wa Kampala-Gongolamboto,Jimbo la Ukonga wilaya ya ilala,jijini Dar es Salaam.

 Akiwa katika viunga vya Kampala-Ukonga,Dkt.Nchimbi amewahutubia Wananchi huku akinadi Sera na Ilani ya chama hicho ya 2025-2030 yenye kulenga kuimarisha na kupeleka maendeleo kwa Wananchi.

 Aidha, baada ya kuhutubia Wananchi,Dkt.Nchimbi pia alipata nafasi ya kuwanadi baadhi ya wagombea Ubunge wa mkoa huo akiwemo mgombea Ubunge wa jimbo la Ukonga,Ndugu Jerry William Silaa, mgombea Ubunge wa jimbo la Kivule Ndugu Dougras Didas Masaburi na Madiwani.

Dkt.Nchimbi ni Mgombea mwenza wa Dkt Samia Suluhu Hassan katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 29, 2025 wakipeperusha bendera ya  Chama   Cha Mapinduzi (CCM), ambapo mkoa wa Dar es Salaam unakuwa wa 15 kufikiwa na Dkt Nchimbi katika kusaka kura za ushindi  wa Kishindo za Mgombea Urais wa chama hicho Dkt.Samia Suluhu Hassan,Wabunge pamoja na Madiwani.







Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top