Skip to main content

Posts

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Mke wa Dk Nchimbi amuombea kura Rais Samia, wabunge Tanga

Mke wa Mgombea mwenza wa CCM, Balozi Dkt Emmanuel Nchimbi Mama Jane Nchimbi akimuombea  kura Rais Samia, wabunge Tanga, leo Jumatatu Septemba 15, 2025 katika Uwanja wa Mazoezi Mjini Korogwe, Tanga. MamaJane Nchimbi ni mwenyeji wa Korogwe alipata fursa hiyo wakati Dk Nchimbi alipokuwa akiendelea na ziara ya kusaka kura mkoani humo.

Dkt.Nchimbi Awasalimu Wananchi Wa Mombo Akiomba Kura Za Ushindi wa Kishindo Kwa Ccm

Mgombea mwenza wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi  (CCM), Dkt. Emmanuel John Nchimbi akiwasalimia wananchi wa Mombo katika Jimbo la Korogwe Vijijini leo Septemba 15, 2025 na kuwaomba kura kwa ajili ya Wagombea wa CCM wa nafasi ya Urais, Ubunge na Madiwani ifikapo Oktoba 29, mwaka huu. DK Nchimbi ameanza siku yake ya kwanza mkoani Tanga kufanya mikutano yake ya kampeni za  Uchaguzi Mkuu wa 2025.

Nitashirikiana na Wana-muheza Kuhakikisha Changamoto Zinaondoka- Mwanafa

Na Mwandishi Wetu, Muheza MGOMBEA ubunge Jimbo la Muheza kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Hamisi Mwinjuma maarufu MwanaFA amesema ataendelea kushirikiana na wananchi wa wilaya ya Muheza kuhakikisha changamoto za Jimbo hilo linafanyiwa kazi. Akizungumza kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika katika kata ya Mkuzi, MwanaFA alisema kuwa changamoto zote zilizopo wilayani hapa anakwenda kuzifanyia kazi kwakuwa ni kipaumbele chake. "Napenda niwahakikishie kuwa changamoto zote za wilaya ya Muheza nakwenda kuzifanyia kazi, hakuna jiwe ambalo litaachwa kugeuzwa...Changamoto zilizopo nakwenda kuzifanyia kazi na zitakuwa kipaumbele changu," alisema mgombea huyo. MwanaFA ambaye ni Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo aliwataka wananchi waende wakapige kura Oktoba 29 na wakawachague wagombea wa CCM kwakuwa katika kipindi cha miaka mitano wamefanya kazi kubwa ya kutekeleza miradi ya maendeleo. Alisema Muheza wamejipanga safari hii kuvunja rekodi ya watu waliojiandikisha kupig...

Michezo Yatajwa Kupunguza Uhalifu Kata Ya Mabatini, Polisi Yapongezwa

Wananchi wa Kata ya Mabatini, Wilaya ya Nyamagana, mkoani Mwanza wamepongeza jitihada za Jeshi la Polisi kuwafikia vijana kwa njia ya michezo, hatua ambayo imesaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza matukio ya uhalifu kwenye kata hiyo. Pongezi hizo zimetolewa Septemba 13, 2025, wakati wa mashindano ya michezo yaliyoandaliwa na Jeshi la Polisi kupitia Mkaguzi Kata wa Mabatini.  Mashindano hayo yalihusisha timu sita za mpira wa miguu kutoka mitaa sita ya kata hiyo ambazo ni; Mabatini Kusini, Mabatini Kaskazini, Majengo Mapya, Nyerere A, Nyerere B na Mbugani B. Katika mchezo wa fainali, timu ya Nyerere A iliibuka mshindi kwa kuifunga Majengo Mapya kwa mabao 2–1 na kukabidhiwa Mbuzi mmoja pamoja na zawadi nyingine. Akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi zawadi kwa washindi, Kaimu Mkuu wa Polisi Wilaya ya Nyamagana Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP) Dastan Kombe, aliwataka wananchi na vijana waendelee kulipa kipaumbele suala la kulinda amani na usalama wa eneo lao.  Alisema awali Kata...

Mzee Makamba amuombea kura Rais Samia,Mgombea ubunge wa CCM Bumbuli

Katibu Mkuu wa CCM mstaafu, Mzee Yusuf Makamba amewaomba wananchi wa Jimbo la  Bumbuli mkoani Tanga kumchagua mgombea urais wa chama hicho, Rais Samia Suluhu Hassan, mgombea ubunge wa jimbo hilo, Mhandisi Ramadhani Singano na madiwani wote wa chama hicho. Makamba amesema hayo leo Septemba 15, 2025 kwa njia ya simu kwenye mkutano wa kampeni za mgombea mwenza wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya chama hicho, Dk Emmanuel Nchimbi uliofanyika Lushoto eneo la Soni. Mzee makamba amesema anaimani na wagombea wote wa CCM na alipenda kuhudhuria mkutano huo ila tatizo ni changamoto ya afya yake. Dk Nchimbi alimpigia simu Mzee Makamba akiwa jukwaani ndipo alipozungumza na kuwaombea kura wagombe wote huku akiwaomba wananchi wa mkoa wa Tanga wasimuangushe katika uchaguzi utakaofanyika Oktoba 29, 2025.

Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa Awapa Kazi Viongozi wa Mkoa wa Kagera

 Na Angela Sebastian; Biharamulo  Kuongozi wa mbio za mwenge Kitaifa Ismail Ali Ussi amewataka mkuu wa mkoa wa Kagera,wakuu wa Wilaya na wakurugenzi wa Halmashauri zote na Manispaa ya Bukoba kuwahamasisha wananchi kutumia Nishati safi ili kuepukana na athari za kiafya zitokanazo na nishati chafu. Ametoa ushauri huo akiwa Wilayani Biharamulo ambapo amesema viongozi hao wanakumbuka kwamba Rais Dk Samia Suluhu Hassan amekuja na kampeni ambayo ina lengo la kuwasaidia wananchi wa Tanzania ikiwemo Biharamulo ambapo inaenda kuwajali na kuwagusa wananchi moja kwa moja kwa kuweka Afya zao kuwa imara. "Dk.Samia amekuja na utaratibu wa uhamasishaji wa matumizi ya gesi na Nishati safi mbadala katika maeneo mbalimbali ndani ya Taifa hili ,ndiyo maana yapo maelezo yaliyotolewa kwa wakuu wa mikoa,Wilaya na wakurugenzi kuwataka wahamasishe kampeni hiyo katika maeneo ambayo yana mkusanyiko wa kuanzia watu 100 na kuendelea ikiwa ni ya binafsi au Serikali kuhakikisha wanatumia gesi ambapo shu...