Skip to main content

Posts

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Sagini Amhakikishia Dkt. Nchimbi Ushindi Wa Asilimia 100 Kutokana na Miradi Iliyopo Butiama

📍JIMBONI BUTIAMA Mbunge wa Jimbo la Butiama na Naibu Waziri Katiba na Sheria Mhe. Jumanne Sagini amemhakikishia Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi kuwa Butiama itaongoza kwa kura za kishindo katika uchaguzi ujao hii kutokana na jinsi Ilani ya CCM ilivyotekelezwa. Akizungumza baada ya Ziara ya Katibu Mkuu wa CCM ya Kutembelea na  kukagua Mradi wa Ujenzi wa Chuo Kikuu cha Mwalimu Julius K. Nyerere cha Kilimo na Teknolojia na Uwekaji wa Jiwe la Msingi kwenye Ujenzi wa Ofisi za CCM Wilaya ya Butiama leo Tarehe 24 Aprili, 2025. Mhe. Sagini amesema kuwa wananchi wamemtuma kumfikishia salamu kuwa wanaimani na CCM hivyo wanajiandaa kupeleka ushindi wa kishindo katika uchaguzi. "Mhe. Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Dkt. Nchimbi kutokana na maendeleo yaliyofanyika hapa Butiama kipindi cha Awamu ya Sita ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kila mwananchi amekiri kweli kazi imefanyika na nimekuwa nikifanya ziara mara kwa mara kila kata ni mabilioni ya fedha yamele...

Musoma Vijijini Wampa Asante Rais Dkt.Samia Ufunguzi Wa Shule Mpya ya Sekondari

Na Shomari Binda-Musoma  WANANCHI wa Jimbo la Musoma Vijijini wametoa asante kwa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuwapatia fedha na kujengwa kwa shule mpya ya sekondari. Asante na shukrani hizo zimeongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Musoma Juma Chikoka,Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini Profesa Sospeter Muhongo na viongozi mbalimbali walioshiriki tukio la ufunguzi wa shule mpya ya Butata sekondari leo aprili 24 2025 Kijiji cha Butata Kata ya Bukima. Akizungumza mara baada ya kutembelea majengo ya shule hiyo yakiwemo madarasa,maabara,jengo la utawala na vyoo Chikoka amesema Rais Samia anastahili asante na shukrani. Chikoka amesema Rais ametoa milioni 584 zilizojenga shule hiyo ambayo imewawezesha watoto kupunguza umbali mrefu wa zaidi ya kilometa 10 kwenda kwenye masomo  Amesema changamoto zilizosemwa kwenye risala likiwemo siala la umeme ametoa maagizo kwa Tanesco kuhakikisha wanafikisha huduma ya umeme ili wanafunzi waweze kusoma vizuri yakiwemo masomo ya sayansi. " Kwa ujenzi wa ...

Tanzania-Canada Kushirikiana Kuendeleza Sekta ya Madini Nchini

▪️Balozi wa Canada apongeza mageuzi makubwa ya sekta ya madini ▪️Wachimbaji wadogo kujengewa uwezo wa uchimbaji madini kwa teknolojia ya kisasa ▪️Mafunzo maalum ya uongezaji thamani kuendeshwa kupitia VETA ▪️Waziri Mavunde asisitiza ushirikiano katika utafiti wa kina wa Madini *Dodoma* Waziri wa Madini Mh. Anthony Mavunde na Balozi wa Canada nchini Tanzania Mh. Emily Burns leo wamekutana Jijini Dodoma na kufanya kikao juu ya maendeleo ya sekta ya madini nchini. Balozi Emily Burns ambaye pia ametumia kikao hicho kwa ajili ya kujitambulisha,amesema nchi ya Canada ipo tayari kushirikiana na Tanzania katika kuwaendeleza wachimbaji wadogo nchini kwa kuwajengeza uwezo katika uchimbaji wa matumizi sahihi ya Teknolojia utakaozingatia utunzaji wa mazingira na kuwajengea ujuzi ili kuongeza tija kwenye uzalishaji madini. Aidha Balozi Burns ameonesha utayari wa serikali ya Canada kutoa mafunzo maalum(_Tailor-made training_) kwa wakinamama na Vijana kupitia vyuo vya Ufundi-VETA katika maeneo ambapo...

Viwanda zaidi ya 4000 kushiriki maonyesho ya EXPO 2025

Na Mwandishi Wetu SHIRIKISHO la Wenye Viwanda Tanzania (CTI), kwa kushirikiana na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE), limezundua Maonesho ya Kimataifa ya Wazalishaji yajulikanayo kama TIMEXPO 2025 Maonyesho hayo yatafanyika kuanzia tarehe 19 hadi 22 Novemba mwaka huu katika ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam na yanatarajiwa kuhudhuriwa na waonyeshaji 4,000 na watembeleaji zaidi ya 35,000. Mgeni rasmi katika uzinduzi huo uliofanyika jana alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Dk Suleiman Serera. Akizungumza wakati wa ufunguzi huo, Dk Serera alisema Tanzania inazidi kupanda chini ya uongozi shupavu na wenye maono ya Rais Samia Suluhu Hassan kwa Serikali kuendelea kutekeleza mageuzi ya kina ili kujenga uchumi wa viwanda wenye ushindani, shirikishi na unaoendeshwa na teknolojia. “Tunawekeza kwenye miundombinu. Tunafanya nishati ya kisasa, kuwezesha biashara, na kuweka dijitali. Tunapunguza gharama za kufanya biashara na kufanya kazi bila kuc...

Balozi Nchimbi akabidhiwa kifimbo mbele ya kaburi la Baba wa Taifa mwl.Julius Kambarage Nyerere

  Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi ametembelea nyumbani kwa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, eneo la MWITONGO  kijiji cha Butiama na kukabidhiwa fimbo maalum na familia hiyo ya mwasisi wa Tanzania na CCM.  Balozi Nchimbi ambaye yuko ziara ya kikazi ya siku tano katika Mkoa wa Mara, mbali ya kukabidhiwa zawadi hiyo, yeye pamoja na msafara wake, pia alipata fursa ya kuweka shada la maua na kufanya misa fupi kwenye kaburi alipozikwa Mwalimu Nyerere.  Kiongozi wa Kabila la Wazanaki, Chifu Japhet Wanzagi, alimwambia Balozi Nchimbi kuwa hicho ni kifaa cha kazi atakachotumia katika dhamana alizoaminiwa kutumikia Watanzania. Alisisitiza kuwa huwa wanafanya hivyo kwa kiongozi mwenye sifa zinazofaa. “Tunakukabidhi fimbo hii. Huwa tunakabidhi kwa kiongozi tunayemkubali. Kwa kuwa huu ni mwaka wa uchaguzi utaitumia kuchapa na kuwarekebisha wale wote ambao wanataka kutatiza shughuli za uchaguzi kinyume na utaratibu wa Kikatiba,” ali...

Waziri Mkuu: Serikali Kuendeleza Mabonde Nchini

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amesema kuwa Serikali inaendelea na mpango wa kuyaendeleza mabonde nchini kwa kuyatumia kutoa huduma za kijamii ikiwemo upatikanaji wa maji na nishati ikiwa ni mkakati wa kukabiliana na mafuriko. Amesema moja ya mkakati uliochukuliwa na Serikali ni kuunda mamlaka za mabonde zenye wajibu wa kufanya ufuatiliaji wa mwenendo upitishaji maji na kuratibu namna nzuri ya utumiaji wa mabonde hayo. Amesema hayo leo (Alhamisi, Aprili 24, 2025) wakati akijibu swali la mbunge wa Kyela, Ally Anyigugile Jumbe aliyetaka kufahamu mpango wa Serikali wa kukabiliana na mafuriko nchini, wakati wa kipindi cha Maswali ya Wabunge kwa Waziri Mkuu. “Kama ambavyo tumeona kwenye bonde la mto Rufiji, tumeamua kuanzisha mradi mkubwa sana wa kuzalisha umeme. Nilifanya ziara mkoani Morogoro ambapo tunachimba bwawa kubwa ambalo linategemea maji ya mto Ruvu; ujenzi wa mabwawa haya yataleta maslahi kwa Watanzania ikiwemo kwenye sekta za kilimo, nishati, maji na mifugo.” Ameongeza kuwa mpango...