Sagini Amhakikishia Dkt. Nchimbi Ushindi Wa Asilimia 100 Kutokana na Miradi Iliyopo Butiama

GEORGE MARATO TV
0


📍JIMBONI BUTIAMA

Mbunge wa Jimbo la Butiama na Naibu Waziri Katiba na Sheria Mhe. Jumanne Sagini amemhakikishia Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi kuwa Butiama itaongoza kwa kura za kishindo katika uchaguzi ujao hii kutokana na jinsi Ilani ya CCM ilivyotekelezwa.

Akizungumza baada ya Ziara ya Katibu Mkuu wa CCM ya Kutembelea na  kukagua Mradi wa Ujenzi wa Chuo Kikuu cha Mwalimu Julius K. Nyerere cha Kilimo na Teknolojia na Uwekaji wa Jiwe la Msingi kwenye Ujenzi wa Ofisi za CCM Wilaya ya Butiama leo Tarehe 24 Aprili, 2025. Mhe. Sagini amesema kuwa wananchi wamemtuma kumfikishia salamu kuwa wanaimani na CCM hivyo wanajiandaa kupeleka ushindi wa kishindo katika uchaguzi.

"Mhe. Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Dkt. Nchimbi kutokana na maendeleo yaliyofanyika hapa Butiama kipindi cha Awamu ya Sita ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kila mwananchi amekiri kweli kazi imefanyika na nimekuwa nikifanya ziara mara kwa mara kila kata ni mabilioni ya fedha yamelelekezwa kutekeleza miradi mbalimbali ikiwemo chuo Kikuu cha Mwl. Julius K. Nyerere cha Kilimo na Teknolojia (MJNUAT), Mradi wa Maji wa Mgango Kiabakari Butiama, Jengo la Halmashauri ya Wilaya ya Butiama, Hospitali ya Wilaya ya Butiama, Chuo cha VETA, Vituo Vitatu vipya ya Afya, Shule za Sekondari 10 na mawasiliano yamefunguka barabara zinapitika," amesema Mbunge Sagini

Katika Ziara hiyo Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi amesema kuwa yote hayo yaliyofanyika Butiama ni kwa sababu ya upendo na uongozi uliotukuka wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye ana maono kama ya Baba wa Taifa Mwl. Julius k Nyerere na uzalendo wa kweli, ndio sababu anaishi na kuenzi falsafa  zake. Ndio maana kaleta mkoani Mara miradi mikubwa mitatu ambayo ni Chuo Kikuu cha Mwl. Julius K. Nyerere cha Kilimo na Teknolojia, Kumbukumbu ya Hospitali ya Mwl. Julius K. Nyerere na Ujenzi wa Uwanja wa Ndege Musoma.

Pia Dkt. Nchimbi amewataka wajumbe wa CCM kusikiliza kauli wananchi pale wanapoenda kupiga kura za ndani ya chama ili walete viongozi ambao ni sahihi na wenye sifa ya kweli siyo wale wanaotaka kugawa wananchi kwa *"UKABILA, UDINI, UTAJIRI NK"* 

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Butiama Ndg. Christopher Siagi amepongeza Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Dkt. Emmanuel Nchimbi kwa ziara yake wilayani Butiama ambayo imeleta hamasa kwa viongozi na wajumbe katika kukiamini chama hiko na kuendelea kuyahubiri yale yaliyo mema yanayotekelezwa na Ilani ya Chama Cha Mapinduzi.








Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top