Skip to main content

Posts

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Mongella Atoa Wito wa Amani Kwa Wana~ccm Uchaguzi Mkuu 2025

Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara, Ndugu John Mongella, amewataka wanachama wa chama hicho kudumisha amani na utulivu kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu. Akizungumza leo, Machi 24, 2025, jijini Arusha kwa niaba ya Katibu Mkuu wa CCM, Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, Mongella amewahimiza wana-CCM kuwa makini na kuepuka vishawishi vinavyoweza kusababisha vurugu. Amesisitiza kuwa huu ni wakati wa kuwa imara, akibainisha kuwa Tanzania ina heshima ya kipekee barani Afrika kutokana na utamaduni wake wa kudumisha amani na utulivu. Katika hotuba yake, Mongella ameipongeza Jumuiya ya Wazazi kwa kuandaa kongamano hilo la kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kutimiza miaka minne ya mafanikio katika uongozi wake. Aidha, ameisifu jumuiya hiyo kwa mikakati yake madhubuti ya kukihami chama na kuhakikisha CCM inapata ushindi katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu.

Watumishi wa Umma wenye Biashara Binafsi Nchini Uganda Wakalia Kuti Kavu

Watumishi wa umma nchini Uganda wanaoendesha biashara za kibinafsi ndani ya sekta zao za kitaaluma sasa wanakabiliwa na matarajio ya athari mbaya, huku serikali ikijiandaa kubana kuanzia Julai 1, 2025. Hatua hiyo ambayo imekuwa mjadala kwa miaka mingi, inalenga kutekeleza uzingatiaji wa kanuni za utumishi wa umma huku serikali ikilenga zaidi sekta za afya na elimu kwa kuanzia. Mara nyingi mijadala juu ya suala hilo imekuwa ikijitokeza, huku walimu wengi walio katika utumishi wa umma wakituhumiwa kutumia muda wao mwingi katika shule binafsi huku madaktari wakitajwa kujihusisha na wizi wa vifaa tiba vya kliniki zao, rufaa zinazotia shaka na utoro kazini. Maafisa kadhaa wa umma katika sekta ya afya wanamiliki hospitali, zahanati, maduka ya dawa na pia wanajishughulisha na ajira za kudumu huko nje. Ni zaidi ya hivyo katika sekta ya elimu ambapo walimu katika shule za umma wamekuwa wakifundisha kwenye shule za kibinafsi huku maafisa kadhaa akiwemo waziri wakiendesha shule zao wenyewe na kus...

Waziri Mkuu Mpya wa Canada aitisha Uchaguzi Mkuu wa Ghafla

  Waziri Mkuu mpya wa Canada, Mark Carney, ametangaza uchaguzi wa dharura Aprili 28,A kisema anahitaji mamlaka madhubuti kushughulikia tishio kutoka kwa Rais wa Marekani, Donald Trump, ambaye “anataka kutuvunja ili Amerika iweze kututawala.” Uhusiano kati ya Amerika na Canada umedorora tangu Trump alipoanzisha ushuru na kutishia kufanya Canada jimbo  la Amerika.  Ingawa uchaguzi ulikuwa umepangwa Oktoba 20, Carney anatumai kutumia kuimarika kwa umaarufu wa chama chake cha Liberal tangu Januari, baada ya Trump kuanza kuitishia Canada na Waziri Mkuu wa zamani Justin Trudeau kujiuzulu. Baada ya kuapishwa Machi 14 mwaka huu, Carney alisema anaweza kushirikiana na Trump, lakini sasa amechukua msimamo mkali zaidi.  “Tunapitia mgogoro mkubwa zaidi wa maisha yetu kwa sababu ya hatua za biashara zisizo za haki za Trump na vitisho kwa uhuru wetu,” alisema baada ya Gavana Mkuu kuidhinisha uchaguzi huo. Ikulu ya Amerika haijajibu mara moja kauli ya Carney. Mnamo Machi 6, Trump a...

Angola Yajiondoa Upatanishi Mgogoro wa Mashariki Mwa Drc

 Rais wa Angola, Joao Lourenço aliteuliwa kuwa mpatanishi na AU mwaka 2022 katika jaribio la kumaliza mzozo unaohusisha M23 ambao ulizidisha mashambulizi yake mwezi Januari na kunyakua maeneo makubwa ya ardhi katika eneo lenye utajiri wa madini mashariki mwa DRC. Rwanda inakanusha kuwapa M23 msaada wa kijeshi. Utawala wa Rais Paul Kagame unasema unakabiliwa na tishio katika eneo hilo kutoka kwa kundi la FDLR, lililoanzishwa na viongozi wa kabila la Wahutu waliohusika katika mauaji ya kimbari ya Watutsi nchini Rwanda mwaka 1994. "Angola inatambua hitaji la kujiondoa kutoka kwa jukumu la upatanishi wa mzozo huu ... ili kuzingatia kwa kina zaidi vipaumbele vya jumla vilivyowekwa na shirika la bara," ilisema Taarifa ya ofisi ya Rais wa Angola.  "Angola daima imekuwa ikiamini katika haja ya mazungumzo ya moja kwa moja kati ya serikali ya DRC na M23," ofisi ya rais iliongeza. Tangu mwisho wa 2021, usitishaji mapigano na mapatano kadhaa yamekubaliwa kabla ya kuvunjwa.  Ang...

Jwtz Yafanya Mazungumzo na Mkuu Jeshi la Nchi Kavu la Afrika Kusini

 Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania Luteni Jenerali Salum Haji Othman amempokea na kufanya mazungumzo na Mkuu wa Jeshi la Nchi Kavu la Afrika ya Kusini Luteni Jenerali Sizakele Charmin Mbatha ofisini kwake Upanga Jijini Dar es Salaam tarehe 24 Machi 2025.  Katika mazungumzo yao, Luteni Jenerali Othman amemthibitishia Mgeni wake kuwa JWTZ litaendeleza mahusiano mema yaliyopo  hususani katika nyanja za oparesheni na mafunzo baina ya nchi hizi mbili ili kuwajengea weledi na utayari makamanda na wapiganaji  kukabiliana na matishio mbalimbali ya kiulinzi na majanga.  Naye, Mkuu wa Jeshi la Nchi Kavu la Afrika  Kusini Luteni Jenerali Sizakele Charmin Mbatha amelishukuru JWTZ kwa mchango wake katika ukombozi wa nchi za kusini mwa Afrika ikiwemo Afrika ya Kusini. Amesema  Afrika ya Kusini inaendelea kuimarisha ushirikiano uliopo kati ya Majeshi ya nchi mbili hizi hususan katika nyanja ya Diplomasia ya Ulinzi. Luteni Jenerali Mbatha na uju...

Kumuombea Kheri Rais Samia ni Uzalendo Kwa Nchi Yetu-kikwete

Wosia huu umetolewa na Mh. Ridhiwani Kikwete , Mbunge wa Chalinze na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana , Ajira na Wenye Ulemavu wakati akiwahotubia Wananchi waliojitokeza kuomba dua kuiombea Nchi na Dr. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nyumbani kwake Msoga, Chalinze.  Akizungumza na umma  wa Watanzania waliojitokeza kwenye dua hiyo, Mh. Kikwete amewashukuru  kwa kujitokeza na kumuombea dua Mh. Rais. “ ukimuombea Rais Samia, umeiombea Tanzania, kutokana na umuhimu wa nafasi yake na yeye akiwa ndiyo mshika maono ya Nchi”. Mh. Kikwete alitumia nafasi hiyo pia kuishukuru serikali ya awamu ya 6 kwa mafanikio makubwa yaliyopatikana katika kipindi cha miaka hii ya Rais Samia Suluhu Hassan ambapo Elimu,Afya, Miundombinu n.k na kutumia nafasi hiyo pia kuwaomba wanachalinze waendelee kumuamini na kumchagua tena kwa kura nyingi.  Wakizungumza baadhi ya masheikh waliohudhuria shughuli hii, wamepokea maombi ya Mbunge wao kwa furaha na hi...