Skip to main content

Posts

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Balozi Dkt Nchimbi Atema Cheche Nchini Ethiopia

  -Asema CCM na PP kuimarisha uhusiano baina ya nchi hizi mbali KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi amesema urafiki kati ya CCM na Prosperity Party, chama tawala cha Ethiopia, ni hatua muhimu katika kuboresha na kuimarisha uhusiano wa nchi hizo mbili, pamoja na watu wake. Balozi Nchimbi amesema kuwa ushirikiano mzuri kati ya Tanzania na Ethiopia umebebwa kwenye misingi imara ya itikadi za kisiasa iliyowekwa na waasisi wa nchi hizo mbili, akitoa wito kuwa uongozi wa kizazi cha sasa unawajibika kuimarisha zaidi kwa ajili ya manufaa ya kiuchumi ya wananchi wa pande zote. Katibu Mkuu wa CCM, Balozi Nchimbi amesema hayo alipokuwa akitoa salaam za CCM kwenye Mkutano Mkuu wa Chama cha PP, uliofanyika mjini Addis Ababa, tarehe 31 Januari 2025, ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kikazi nchini Ethiopia. “Kwa niaba ya Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, tunawapongeza sana wenzetu wa Prosperity Party,...

Waziri Mkuu Amesema Tanzania Imejipanga Vema Katika Maandalizi ya Chan na Afcon

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema Serikali imejipanga vyema kukamilisha maandalizi yote muhimu ikiwemo miundombinu kwa ajili ya Michuano ya Mpira wa Miguu kwa Nchi za Africa CHAN na AFCON. "Tanzania imejipanga vizuri, kuhakikisha kuwa michuano hii inafanyika hapa Nchini, Serikali inawajibika kuhakikisha inaandaa viwanja na miundombinu mingine."  Ameyasema hayo leo (Jumamosi Februari Mosi, 2025) aliposhiriki katika Tamasha la Michezo la Bunge Bonanza lililofanyika kwenye Viwanja vya Shule ya Sekondari ya John Merlin jijini Dodoma. Amesema kuwa tayari ukaguzi wa baadhi ya viwanja umefanyika na vimeonekana kukidhi vigezo “Viwanja vilivyokaguliwa vipo Tanzania bara na Visiwani, na kazi bado inaendelea, lengo ni kuhakikisha michuano hii inafanyika kwa ufanisi” Mheshimiwa Majaliwa amesema ni vyema sasa Watanzania wakajipanga kutumia fursa zitakazo jitokeza kutokana na kuwepo kwa michuano hiyo hapa Nchini. "Hii ni fursa kwetu Watanzania, lazima tujipange kutumia fursa za kiu...

Rais Samia aungana na Wakuu wa Nchi za Sadc Katika Mkutano wa Dharura Nchini Zimbabwe

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC-Organ) Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akishiriki Mkutano wa Dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa SADC katika ukumbi wa New Parliament Building, Harare nchini Zimbabwe tarehe 31 Januari, 2025. Mkutano huo pamoja na mambo mengine unajadili hali ya ulinzi na usalama Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC-Organ) Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na  baadhi ya Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika SADC kabla ya kuanza kwa Mkutano wao wa  Dharura uliofanyika katika ukumbi wa New Parliament Building, Harare nchini Zimbabwe tarehe 31 Januari, 2025.  Matukio mbalimbali wakati wa Mkutano wa Dharura wa Wak...

Ccm Kimbilio La Wananchi, Tujadili Mambo Yanayowahusu - Wasira

Na Mwandishi Wetu, Bunda MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Stephen Wasira, amesema Chama ni kimbilio la wananchi hivyo lazima kijadili na kubeba shida za watu. Ameagiza vikao vya Chama vizungumzie mambo yanayowahusu wananchi kwa lengo la kusikia changamoto zao na kuwa sehemu ya kupatiwa ufumbuzi. Wasira alieleza hayo mjini Bunda leo Januari 31, 2025 alipokutana na kuzungumza na wafanyabiashara na wajasiriamali wa Wilaya ya Bunda mkoani Mara. Amesisitiza kuwa siyo sahihi vikao hivyo kujadili mambo yasiyo na maana wakati wananchi kjatika maeneo husika wanakabiliwa na changamoto ambazo endapo zitasikilizwa na kufikishwa mbele ya mamlaka husika zitapatiwa ufumbuzi. “CCM ni lazima isikilize watu wanataka nini, sisi ni Chama cha watu na kwa kweli tunataka kiwe cha watu kwelikweli, vikao vyetu vya CCM vizungumze mambo ya watu, kama ni mambo ya wafanyabiashara wadogowadogo (machinga) tuzungumze kuhusu hilo, kama wana matatizo wakimbilie CCM kwa sababu wanajua huko n...

Rais Samia Awasili Nchini Zimbabwe

 Matukio mbalimbali ya kuwasili kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Robert Mugabe, Harare nchini Zimbabwe kwa ajili ya kuhudhuria Mkutano wa Wakuu wa nchi wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) unaofanyika leo tarehe 31 Januari, 2025.

Tls Mkoa wa Mara Wataka Mahakama Kupewa Uwezo wa Kutoa Amri ya Kukamata Mali za Serikali

Na Ada Ouko, Musoma. CHAMA cha wanasheria wa kujitegemea(TLS) Mkoani Mara kimeiomba Serikali, kufanya Marekebisho ya Sheria inayotoa Hukumu dhidi ya Serikali ili kutengeneza usawa wa haki. Ombi hilo limetolewa na Wakili wa kujitegemea wa Chama hicho wilayani hapa Daud Mahemba alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kwenye Maadhimisho ya Wiki ya Sheria yaliyozinduliwa na Mkuu wa Mkoa huo Evans Mtambi January 25 Mwaka huu. "Ikitokea Mwananchi ameshinda kesi dhidi ya Serikali Mahakama haina mamlaka ya kisheria ya kutoa amri ya kukamata mali ya serikali moja kwa moja kupitia dalali wa Mahakama"alisema. Mahemba alisema utaratibu uliopo ni kuiandikia serikali kupitia hazina ilipe deni ambapo Afisa Masuhuli wa serikali haitekelezi hukumu hiyo kwa madai ya kuwa serikali haina fedha na kwamba mwananchi aliyeshinda kesi hutembea na hukumu isiyotekelezeka kwa muda mrefu. Alisema mdai akimpeleka mahakamani afisa masuhuli kwa lengo la kufikishwa gerezani kwa kosa la kushindwa kutekel...