Tls Mkoa wa Mara Wataka Mahakama Kupewa Uwezo wa Kutoa Amri ya Kukamata Mali za Serikali

GEORGE MARATO TV
0


Na Ada Ouko, Musoma.

CHAMA cha wanasheria wa kujitegemea(TLS) Mkoani Mara kimeiomba Serikali, kufanya Marekebisho ya Sheria inayotoa Hukumu dhidi ya Serikali ili kutengeneza usawa wa haki.

Ombi hilo limetolewa na Wakili wa kujitegemea wa Chama hicho wilayani hapa Daud Mahemba alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kwenye Maadhimisho ya Wiki ya Sheria yaliyozinduliwa na Mkuu wa Mkoa huo Evans Mtambi January 25 Mwaka huu.

"Ikitokea Mwananchi ameshinda kesi dhidi ya Serikali Mahakama haina mamlaka ya kisheria ya kutoa amri ya kukamata mali ya serikali moja kwa moja kupitia dalali wa Mahakama"alisema.

Mahemba alisema utaratibu uliopo ni kuiandikia serikali kupitia hazina ilipe deni ambapo Afisa Masuhuli wa serikali haitekelezi hukumu hiyo kwa madai ya kuwa serikali haina fedha na kwamba mwananchi aliyeshinda kesi hutembea na hukumu isiyotekelezeka kwa muda mrefu.

Alisema mdai akimpeleka mahakamani afisa masuhuli kwa lengo la kufikishwa gerezani kwa kosa la kushindwa kutekeleza hukumu wakati hujitetea kwa kusema kuwa serikali haina fedha hali inayopelekea usumbufu kwa mdai.

Mary Joakimu mbaye pia ni wakili wa kujitegemea kupitia chama hicho alisema tofauti na kesi nyingine za kawaida ikitokea mdai ameshinda, Mahakama huteua dalali nae huenda kukamata mali ya mdaiwa na mhusika anapata stahiki yake.

" Kwa upande wa serikali kwa mujibu wa sheria huwezi kukamata mali ya serikali na badala yake hutumika njia ya kuiandikia Serikali ili iweze kulipa fidia kupitia kwa afisa masuhuli" alisema Mary.

Aidha mawakili hao wametoa wito kwa wananchi kutumia fursa hii ya maadhimisho ya wiki ya sheria kutembelea mabanda yanayotoa elimu ya sheria kwa kuwa huduma hiyo inatolewa bila malipo yoyote.

Maadhimisho hayo yanatarajiwa kufikia kilele february 3 mwaka huu na kwamba kauli mbiu Inasema" Tanzania ya 2050: Nafasi ya Taasisi zinazosimamia Haki Madai Katika Kufikia Malengo Makuu Ya Dira ya Taifa ya Maendeleo.














Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top