Skip to main content

Posts

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Dkt. Biteko ainadi Ccm Mara Kimkakati

📌 Asema CCM Inaweza Kazi, Ipewe Kura 📌 Wabunge Waeleza Mafanikio ya CCM Mara 📌 Wagombea Uenyeviti Wajinadi kwq Wananchi 📌 Wananyamongo Wahaidi Ushindi CCM Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa ambaye pia ni Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amewataka wananchi wa Nyamongo  na Mkoa wa Mara kwa ujumla kufanya kampeni za kistaarabu na kujitokeza kupiga kura katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaofanyika Novemba  27, 2024. Dkt. Biteko ameeleza  kuwa  maendeleo hayaletwi  kwa matuso wala kuvunjiana heshima na kuwa wananchi hao washinde ubaya kwa wema. Aidha, wamefika  eneo hilo kwa lengo la kuwaomba wananchi wa Nyamongo wachague watu ambao wataungana na Serikali katika kuwaletea maendeleo. Dkt. Biteko  ameyasema hayo leo Novemba 20, 2024 wakati akifungua kampeni  za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa Mkoa wa Mara zilizofanyika m katika Uwanja Nyamongo Wil...

Biteko apokelewa Mkoani Mara kwa Kishindo

Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa ambaye pia ni Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko akivalishwa skafu na Kijana wa Hamasa na Itifaki Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Mara, Godwin Gudluck Bunyoga  wakati wa mapokezi alipowasili Mkoani Mara. Mh Biteko amewasili mkoani Mara kwa ajili ya uzinduzi wa Kampeni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa katika Mkoa wa Mara uliofanyika Novemba 20, 2024 katika uwanja wa nyangoto Stendi - Nyamongo Wilaya ya Tarime.

Rais Dkt. Samia asisitiza nchi za Sadc Kumaliza Migogoro

Mwenyekiti wa asasi ya siasa, ulinzi na usalama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan amezisisitiza  nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika SADC kuunga mkono juhudi za kidiplomasia za kumaliza Uhasama uliopo baina ya DRC na Rwanda chini ya mchakato wa Angola. Rais Dk.Mwinyi ameyasema hayo kwa niaba ya Rais Dkt.Samia alipomwakilisha kufungua Mkutano wa  Viongozi Wakuu  na Serikali wa  Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika uliofanyika jijini Harare Zimbabwe tarehe 20 Novemba 2024. Rais Dk, Samia amefafanua kuwa wakati nchi za SADC zikiendelea kujadili hali ya  Usalama wa Mashariki ya  DRC ni vyema kukawekwa mifumo imara ya Ufuatiliaji na utekelezaji wa maazimio  yanayoidhinishwa na  Jumuiya mbalimbali za Kikanda ikiwemo  yale ya Umoja wa Afrika(AU) na Umoja wa Mataifa (UN). Ameeleza kuwa hatua hiyo itawezesha kupatikana kwa Misaada ya kifedha na kilojistik...

Waziri Kikwete akutana na Balozi wa Japan nchini

  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Ridhiwani Kikwete amekutana na kuzungumza na Balozi wa Japan nchini Tanzania. Balozi huyo ambaye pia ni Mwakilishi wa Japan katika Jumuiya ya Afrika Mashariki, Mhe. Yusushi Misawa pamoja na ujumbe wake amepomtembelea waziri Kikwete katika Ofisi ya NSSF, Jijini Dar es Salaam. Katika kikao hicho, wamejadili mambo mbalimbali ikiwemo kuwezesha vijana wa Kitanzania nafasi za kujifunza kazi na kuimarisha mafunzo pamoja na kuongeza ujuzi.

Zahanati ya Nyasaungu Kuanza Kutoa Huduma za Afya Mwezi December 2024

Fresha Kinasa,  Mara. KIJIJI  cha Nyasaungu  chenye vitongoji vitano (5) kilichopo katika Wilaya ya Musoma Mkoani Mara  kinakamilisha ujenzi wa zahanati yake ambayo inatarajiwa kuanza kutoa Huduma za Afya kwa Wananchi  ifikapo Disemba 2024.   Hayo yamebainishwa kupitia taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Mbunge wa Jimbo hilo Novemba 18, 2024.  Kikiwa ni  moja ya vijiji vitatu vya Kata ya Ifulifu ambapo  Vijiji vingine ni Kabegi na Kiemba ambavyo kila kimoja kina zahanati yake. Kufuatia hatua hiyo, ifikapo Disemba 2024, kila kijiji ndani ya Kata ya Ifulifu kitakuwa na zahanati yake. Hatua  ambayo imetajwa kuwa kubwa sana ya maendeleo kwenye Kata hiyo.  Zahanati hiyo ujenzi wake ulianza  kwa kutumia michango ya fedha kutoka kwa wanakijiji na Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo. Ambapo aliendesha Harambee mbili za kupata fedha za kuanza ujenzi wa zahanati hiyo na Wanakijiji wanachangia nguvukazi kwenye ujenz...

Waziri Mkuu amesema Serikali itaendelea Kuboresha Mazingira ya Uwekezaji Nchini

*Lengo ni kuwezesha sekta hiyo kuendelea kuongeza mchango katika ukuaji uchumi WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali itaendelea kuweka mazingira wezeshi kwa wawekezaji wakubwa na wadogo kwenye sekta ya madini ili kuhakikisha wanaendesha shughuli zao kwa tija na kusaidia kukuza uchumi wao na wa Taifa kwa ujumla. Amesema lengo ni kuwezesha sekta hiyo inaendelea kuongeza mchango wake katika ukuaji wa uchumi wa nchi kwa kuhakikisha inachangia zaidi ya asilimia 10 katika pato la Taifa ifikapo 2025. “Hii ni pamoja na kuendelea kuboresha miundombinu ya umeme, barabara, reli, bandari na viwanja vya ndege ili kusaidia shughuli za madini kufanyika kwa tija na kwa gharama nafuu.“ Waziri Mkuu ameyasema hayo leo  (Jumanne, Novemba 19, 2024) alipomwakilisha Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Mkutano wa Kimataifa wa Madini na Uwekezaji Tanzania unaofanyika kwenye Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere, Dar es Salaam. Amesema lengo la mkutano huo ni pamoja na kuvut...