Zahanati ya Nyasaungu Kuanza Kutoa Huduma za Afya Mwezi December 2024

GEORGE MARATO TV
0



Fresha Kinasa,  Mara.

KIJIJI  cha Nyasaungu  chenye vitongoji vitano (5) kilichopo katika Wilaya ya Musoma Mkoani Mara  kinakamilisha ujenzi wa zahanati yake ambayo inatarajiwa kuanza kutoa Huduma za Afya kwa Wananchi  ifikapo Disemba 2024.  

Hayo yamebainishwa kupitia taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Mbunge wa Jimbo hilo Novemba 18, 2024.  Kikiwa ni  moja ya vijiji vitatu vya Kata ya Ifulifu ambapo  Vijiji vingine ni Kabegi na Kiemba ambavyo kila kimoja kina zahanati yake.

Kufuatia hatua hiyo, ifikapo Disemba 2024, kila kijiji ndani ya Kata ya Ifulifu kitakuwa na zahanati yake. Hatua  ambayo imetajwa kuwa kubwa sana ya maendeleo kwenye Kata hiyo. 

Zahanati hiyo ujenzi wake ulianza  kwa kutumia michango ya fedha kutoka kwa wanakijiji na Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo. Ambapo aliendesha Harambee mbili za kupata fedha za kuanza ujenzi wa zahanati hiyo na Wanakijiji wanachangia nguvukazi kwenye ujenzi wa zahanati yao.

Ambapo pia, Serikali kuu imechangia Mil. 100, na Jengo kuu la Zahanati linakamilishwa, Choo chenye matundu matatu kinajengwa. Na Mkandarasi amepewa mkataba wa kukamilisha ujenzi wa Zahanati hii (jengo kuu na choo) unaoishia tarehe 30 Novemba 2024.

Taarifa hiyo umesema Wananchi wa Kijiji cha Nyasaungu wanaendelea kuishukuru serikali pamoja Mbunge wao kwa kuendelea Kuimarisha huduma  muhimu lakini pia kujitolea kwao nguvu kazi kunaharakisha maendeleo ya Kijiji chao. 

"Shule ya msingi ipo, Sekondari inajengwa na imepangwa kufunguliwa mwakani, 2025. Zahanati inajengwa na imepangwa kufunguliwa Disemba 2024, pia Serikali inaendelea kuwasambazia maji ya bomba kutoka Ziwa Victoria, na umeme wa REA."imeeleza sehemu ya taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Mbunge.  

Kwa upande wake Beatha Masatu Mkazi wa Nyasaungu amesema, Wananchi wa Kijiji hicho wanamatumaini, furaha na shauku kubwa kuona huduma za afya zikianza kutolewa Karibu na makazi yao.  

Naye Veronica Mafuru amesema, mbali na Zahanati hiyo kujengwa, lakini pia ameshukuru juhudi zilizofanywa na Mbunge wa Jimbo hilo Prof. Muhongo akishirikiana na Serikali inayoongozwa na Dkt.  Samia Suluhu Hassan kutekeleza miradi mbalimbali iliyogusa elimu, afya na Maji kwa kiwango kikubwa.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top