Skip to main content

Posts

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

RAIS SAMIA KUELEKEA ETHIOPIA KUZINDUA MPANGO WA KUBORESHA AFYA YA MAMA NA MTOTO AFRIKA

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, leo Novemba 22, 2026, anaondoka nchini kuelekea Addis Ababa, Ethiopia, kwa ziara ya kikazi ya siku mbili, itakayomuweka katika nafasi muhimu ya kushiriki juhudi za kikanda za kuboresha afya ya mama na mtoto barani Afrika. Akiwa Kinara wa Umoja wa Afrika wa Afya ya Uzazi, Mama na Mtoto, Rais Dkt. Samia anatarajiwa kushiriki Mkutano wa Tano wa Kimataifa wa Afya ya Umma Barani Afrika (CPHIA 2026), pamoja na kuzindua Mpango Elekezi wa Kuboresha Afya ya Mama na Mtoto Barani Afrika, utakaofanyika Novemba 23, 202 Mpango huo unalenga kuimarisha juhudi za nchi wanachama wa Umoja wa Afrika katika kufikia malengo makuu matatu yanayofahamika kama Sifuri Tatu (Three Zeros), ambayo ni kuhakikisha kila mjamzito anajifungulia katika kituo cha kutolea huduma za afya chini ya uangalizi wa mtaalamu, kutokomeza vifo vya mama wajawazito na watoto wachanga vinavyoweza kuzuilika, pamoja na kuhakikisha kila mtoto anapata hudum...

DKT. MWIGULU ASEMA MIGOGORO YA ARDHI ISICHOCHEE VISASI*

  *_▪ Aonya dhidi ya kujichukulia sheria mikononi na kuuza ardhi kinyemela_* *_▪ Serikali yakamilisha usanifu wa barabara ya njia sita kutoka Picha ya Ndege hadi Chalinze_* WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba, amekemea tabia ya watu kujichukulia sheria mkononi na kuonya kuwa Serikali haiungi mkono uvunjaji wa sheria wa makusudi. “Tusiruhusu uvunjifu wa sheria wa makusudi kwa sababu utaua udugu wetu uliokuwepo kwa miaka mingi. Lazima tuzingatie utawala wa sheria, tuache utaratibu wa uvunjifu wa sheria na kujichukulia sheria mkononi,” amesisitiza. Akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Viwanja vya Polisi, wilayani Chalinze, mkoani Pwani, jana jioni (Jumamosi, Novemba 21, 2026), Waziri Mkuu alisema mmomonyoko wa utawala wa sheria unaalika visasi na makovu yasiyopona. “Tusibaguane au kuchukiana kwa sababu ya ardhi kwani yenyewe haiongezeki lakini mahitaji ya ardhi yanaongezeka. Tunatakiwa tuweke nguvu kubwa katika kupanga matumizi bora ya ardhi na tuheshimu ...

GEORGE MARATO TV YABAINISHA UKWELI KUHUSU TAARIFA YA WALIMU KWIMBA KUFUNDISHA HADI DESEMBA 20

  Kufuatia taarifa iliyochapishwa na chombo kimoja cha habari na kusambaa katika mitandao ya kijamii, ikidai kuwa walimu wa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba wameagizwa kuendelea kufundisha hadi Desemba 20, uchunguzi uliofanywa na George Marato TV umebaini kuwa taarifa hiyo si sahihi na haioneshi uhalisia wa utaratibu unaotekelezwa katika halmashauri hiyo. Uchunguzi umebaini kuwa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba haiendelezi shughuli za ufundishaji wakati wa likizo za shule, isipokuwa wanafunzi hupangiwa zamu maalumu za kushiriki katika shughuli za usafi wa mazingira ya shule pamoja na kuhudumia mashamba ya shule yanayozalisha chakula kwa ajili ya matumizi yao. Aidha, taarifa iliyochapishwa na chombo hicho cha habari ilidai kuwa mdau mmoja wa elimu alikuwa ameitaka Idara ya Elimu ya Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba kuingilia kati agizo hilo linalodaiwa kutolewa, kuchunguza utaratibu wa malipo ya walimu na kuhakikisha walimu pamoja na wanafunzi wanapata likizo kwa mujibu wa miongozo iliy...

MBUNGE MGORE: TANZANIA KUCHOTA UZOEFU ITALIA KUKUZA SEKTA YA RELI KWA DIRA YA RAIS SAMIA

  Mbunge wa Jimbo la Musoma Mjini, Mhe. Mgore Miraji Kigera, akiwa katika ziara ya kikazi nchini Italia, ametembelea eneo la Balzona ambako ujenzi wa handaki (Tunnel) la reli unaendelea, ikiwa ni sehemu ya kujifunza teknolojia, ubunifu na mifumo ya kisasa inayotumika kuendeleza miundombinu ya reli. Mradi huo, wenye thamani ya takribani Euro bilioni 11, ni miongoni mwa uwekezaji mkubwa katika sekta ya reli nchini Italia, huku Serikali ya Italia ikichangia asilimia 50 ya gharama za utekelezaji wake. Ujenzi wa handaki hilo unalenga kurahisisha usafiri wa treni, kupunguza muda wa safari na kuongeza ufanisi wa usafirishaji wa abiria na mizigo, jambo linaloonesha umuhimu wa kuwekeza katika miundombinu ya kisasa ya reli kama kichocheo cha maendeleo ya kiuchumi. Ziara hiyo ina umuhimu wa kimkakati kwa Tanzania katika kuimarisha ushirikiano wa kimataifa, kujifunza teknolojia na kupata uzoefu wa nchi zilizoendelea katika uwekezaji wa reli. Pia, inaendana na dhamira ya Serikali inayoongozwa n...
  Mheshimiwa Waziri wa Ulinzi na JKT ameshiriki katika sherehe za kuwatunuku kamisheni, Maafisa Wanafunzi kundi la 07/23 , shahada ya sayansi ya Kijeshi na kundi la 73/25-Regular pamoja na Mahafali ya Saba ya shahada ya sayansi ya Kijeshi ya kundi 07/23 katika Chuo cha Mafunzo ya kijeshi (TMA) Monduli Mkoani Arusha, tarehe 21 Novemba, 2026. Ambapo Mgeni rasmi akiwa ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan

RAIS SAMIA AKISALIMIANA NA VIONGOZI MARA BAADA YA KUWASILI TMA MONDULI

  Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na Amiri Jeshi Mkuu, akisalimiana na viongozi mbalimbali baada ya kuwasili katika Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi (TMA) Monduli mkoani Arusha, tarehe 21 Novemba, 2026, kwa ajili ya kuwatunuku Kamisheni, Maafisa Wanafunzi kundi la 07/23- Shahada ya Sayansi ya Kijeshi na Kundi la 73/25- Regular pamoja na Mahafali ya saba ya Shahada ya Sayansi ya Kijeshi kwa kundi la 07/23