Baada ya trilioni 2.44 za mwaka wa fedha 2025/2026, wizara ya Elimu kufungua pazia la bajeti mpya kesho Mei 07, 2026 Leo Mei 06, 2026, Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Wanu Hafidhi Ameir amewasilisha Bungeni jijini Dodoma randama za makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2026/ 2027 ikiwa ni hatua ya awali kuelekea hotuba rasmi hapo kesho Mei 07, 2026 Ikumbukwe kwamba Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia katika bajeti iliyopita iliomba na kuidhinishiwa Sh trilioni 2.44 kwa mwaka 2025/2026, sasa macho yote yako kwenye bajeti ya 2026/2027 inayotarajiwa kuwasilishwa bungeni kesho.
Marato tv - Sauti ya Jamii