Na Thomas Lutego ; Misungwi
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi Bi.Peniel Titus ambaye pia ni Mkuu wa Idara ya Mipango wa Halmashauri hiyo amefungua Mafunzo ya MMI na Amesisitiza Umuhimu wa Mafunzo Hayo kwa Wakuu wa Idara na Vitengo kwani ndio Sehemu za kujibu Hoja za CAG ambapo Mafunzo hayo ni Muhimu kwa Halmashauri Katika kutekeleza Shughuli mbalimbali za Miradi.
Mkufunzi wa MMI Mkoa wa Mwanza Bw. Kusire Swai ameeleza kuwa Mafunzo hayo ni Marefu hivyo yanahitaji Umakini Na Ufuatiliaji.
Hivyo ni Vyema Kufuata Sheria,Kanuni,Taratibu na Miongozo na ni Muhimu Mafunzo haya Wapewe wakuu wa Idara na Vitengo kwani Mafunzo haya ya hoja ni Muhimu kwani chanzo cha hoja ni kuanzisha Mradi na ndio wahusika wa hoja.
Amesisitiza kwa Sasa Hoja zote zitajibiwa kwenye Mfumo ambao Umeboreshwa na TAMISEMI.





Comments
Post a Comment