Skip to main content

Posts

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Katibu Mkuu CCM Aongoza Kikao Cha Sekreterieti-Zanzibar

 Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Asha-Rose Migiro akiongoza Kikao cha Sekreterieti ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, leo Jumamosi, tarehe 24 Januari,2026, Afisi Kuu ya CCM, Kisiwandui, Zanzibar.

Serikali Imedhamiria Kupeleka Fursa Kwa Vijana Vijijini Kwa Kuanzisha Mitaa ya Viwanda

DODOMA, JANUARI 24, 2026 SERIKALI wizara ya viwanda na Biashara imeweka mkazo mpya katika kuleta viwanda karibu na wananchi kupitia mitaa ya viwanda na kongani kwa lengo la kufungua milango Kwa vijana kumiliki viwanda na Biashara zao ili kujipatia kipato. Kauli hiyo ameitoa waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Judith Kapinga leo Januari 24,2026 Jijini Dodoma wakati akieleza ahadi za Rais Dkt. Samia Suluhu Hassani katika kipindi Cha siku mia Moja za uongozi wake baada ya uchaguzi Mkuu. Amesema utekelezaji huo wa uendelezaji wa mitaa ya viwanda na programu ya vijana kipato cha wakulima kinaongezeka kupitia uboreshaji thamani, na maelfu ya vijana wanafungua milango ya kuwekeza viwanda na biashara ndani ya kampuni hiyo. "Tathmini ya awali ya kongani na mitaa ya viwanda imekamilika katika mikoa 11 nchini ikibainisha uwezo wa ujasiriamali na maeneo yenye uongezaji thamani ya mazao". Amesema  Aidha,waziri Kapinga amesema serikali imekamilisha mchakato wa kufunga Kiwanda cha kuchakata ...

Serikali Imedhamiria Kupeleka Fursa Kwa Vijana Vijijini Kwa Kuanzisha Mitaa ya Viwanda

DODOMA,JANUARY 24,2026 SERIKALI kupitia wizara ya viwanda na Biashara imeweka mkazo mpya katika kuleta viwanda karibu na wananchi kupitia mitaa ya viwanda na kongani kwa lengo la kufungua milango Kwa vijana kumiliki na kuendesha viwanda na Biashara zao ili kujipatia kipato. Kauli hiyo ameitoa waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Judith Kapinga leo January 24,2026 Jijini Dodoma wakati akieleza ahadi za Rais Dkt. Samia Suluhu Hassani katika kipindi Cha siku mia Moja za uongozi wake baada ya uchaguzi Mkuu. Amesema utekelezaji huo wa uendelezaji wa mitaa ya viwanda na programu ya vijana kipato cha wakulima kinaongezeka kupitia uongezaji thamani, na maelfu ya vijana wanafunguliwa milango ya kumiliki na kuendesha viwanda na biashara ndani ya kongani hizo. "Tathmini ya awali ya kongani na mitaa ya viwanda imekamilika katika mikoa 11 nchini ikibainisha mahitaji ya wajasiriamali na maeneo yenye uwezo mkubwa wa uongezaji thamani wa mazao". Amesema  Aidha,waziri Kapinga amesema serikali i...

Wahitimu wengi NIT wanapata ajira baada ya kuhitimu

Na Mwandishi Wetu CHUO cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), kimesema tafiti zinazofanywa kwa wahitimu wa chuo hicho zinaonyesha kuwa wahitimu wa chuo hicho wamekuwa wakipata ajira na kujiajiri kutokana na umahiri wanaotoka nao chuoni hapo. Hayo yalisemwa jana chuoni hapo na Mkurugenzi wa Taaluma wa chuo hicho,Eva Omari wakati wa kongamano la kuwapa ujuzi wahitimu wa chuo hicho mwaka huu, kuhusu mambo yanayohitajika kwenye jira. Kwenye kongamano hilo wataalamu kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu walitoa mada mbalimbali  za kuwapa ujuzi zaidi wahitimu hao kuhusu namna ya kujitambulisha, kujiamini na namna ya kuenenda baada ya chuo. Eva alisema wanafunzi wanaopewa ujuzi ni wanafunzi wa mwaka wa tatu ambao wanatarajiwa kuhitimu kozi mbalimbali na kuingia kwenye soko la ajira kufanya kwa vitendo yale waliyofundishwa chuoni. “Tuko hapa na wataalamu mbalimbali kuhakikisha wanawapa ujuzi ili wanapoingia kwenye soko la ajira hawababaiki, ingawa wamekaa chuo kwa miaka mitatu lakini kuna ujuzi ambao ni ...

Dkt. Mwigulu Atoa Heshima za Mwisho Kwa Mwili wa Mzee Mtei

Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT), marehemu Mzee Edwin Isaac Mtei, Nyumbani kwa marehemu Tengeru (Chama), Wilaya ya Arumeru Mashariki mkoani Arusha, Januari 24, 2026. Mheshimiwa Dkt. Mwigulu anamwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan katika mazishi ya Mzee Edwin Issac Mtei.

Dkt. Mwigulu Asaini Kitabu Cha Maombolezo ya Msiba wa Mzee Edwin Mtei

Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba akitia saini kitabu cha maombolezo ya msiba wa  aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT), marehemu Mzee Edwin Isaac Mtei, Nyumbani kwa marehemu Tengeru (Chama), Wilaya ya Arumeru Mashariki mkoani Arusha, Januari 24, 2026. Dkt. Mwigulu ameongozana na Mkewe Neema Mwigulu. Mheshimiwa Dkt. Mwigulu anamwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan katika mazishi hayo.