DODOMA, JANUARI 24, 2026
SERIKALI wizara ya viwanda na Biashara imeweka mkazo mpya katika kuleta viwanda karibu na wananchi kupitia mitaa ya viwanda na kongani kwa lengo la kufungua milango Kwa vijana kumiliki viwanda na Biashara zao ili kujipatia kipato.
Kauli hiyo ameitoa waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Judith Kapinga leo Januari 24,2026 Jijini Dodoma wakati akieleza ahadi za Rais Dkt. Samia Suluhu Hassani katika kipindi Cha siku mia Moja za uongozi wake baada ya uchaguzi Mkuu.
Amesema utekelezaji huo wa uendelezaji wa mitaa ya viwanda na programu ya vijana kipato cha wakulima kinaongezeka kupitia uboreshaji thamani, na maelfu ya vijana wanafungua milango ya kuwekeza viwanda na biashara ndani ya kampuni hiyo.
"Tathmini ya awali ya kongani na mitaa ya viwanda imekamilika katika mikoa 11 nchini ikibainisha uwezo wa ujasiriamali na maeneo yenye uongezaji thamani ya mazao". Amesema
Aidha,waziri Kapinga amesema serikali imekamilisha mchakato wa kufunga Kiwanda cha kuchakata zao la Muhogo mbichi kupata unga wa muhogo katika Halmashauri ya Wilaya ya Handeni Tanga.
"Kufungwa Kwa mtambo huu kutawezesha kukausha tani kumi na mbili (12) za muhogo mbichi kwa saa kumi (10) na kutoa tani 3 za unga wa muhogo". Amesema
"Mradi unatoa ajira 150 za moja kwa moja na zaidi ya ajira 300 zisizo za moja kwa moja kwa vijana na akina mama wa maneno yao la muhogo". Ameongeza
Kadhalika,Waziri Kapinga amesema katika viwanda nchini serikali imeshaanza mchakato wa Kuainisha maeneo yenye madini muhimu ya kimkakati (critical minerals) nchini, ikijumuisha yale yanayohitajika katika viwanda vya teknolojia, jadidifu na teknolojia ya teknolojia.
"Utafiti huu wa kina wa madini muhimu tumeanza na Wilaya ya Kyerwa, Mkoa wa Kagera,Wilaya ya Ikungi, Mkoa wa Singida". Amesema
" na tutafanya kazi za uhamasishaji na ushirikishaji wa jamii katika maeneo husika kuhusu uchimbaji salama, ulinzi wa mazingira, afya na fursa za biashara zinazotokana na shughuli za utafiti na uchimbaji". Amesisitiza
Katika kutekeleza na kuimarisha amani ya nchi, Msemaji mkuu wa serikali na katibu Mkuu wa wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Gerson Msigwa amewaasa vijana kote nchini mstari wa mbele kuilinda na kuidumisha Amani iliyopo nchini.
"Serikali imeshaweka Miundombinu Rafiki kwenu vijana,hivyo mnapaswa Kulinda Amani hii tuliyonayo". Amesema
Sekta ya Viwanda na Biashara imeonesha thabiti na wa mbele katika mambo makuu Mbalimbali ikijumuisha Mikopo 193 yenye thamani ya zaidi ya Shilingi milioni 820 imetolewa na ajira 546 nyingi kwa vijana.














Comments
Post a Comment