Skip to main content

Posts

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Wananchi Rufiji wampongeza Mhe. Mchengerwa utekelezaji wa miradi ya Maendeleo

 OR-TAMISEMI WANANCHI wa Rufiji mikoani Pwani wameeleza kufurahishwa na utekelezaji wa miradi ya maendeleo jimboni humo ikiwemo ujenzi wa barabara, zahanati, shule, madaraja na zahanati. WANANCHI hao pia wamempongeza Mbunge wa Rufiji, Mhe. Mohamed Mchengerwa kwa jitihada zake za kuhakikisha huduma za jamii zinapatikana kwa uhakika na ubora. Wameyasema hayo kwa nyakati tofauti wakati wa ziara ya kikazi ya Mwenyekiti wa UWT taifa Mhe. Mary Pius Chatanda aliyoifanya Wilayani Rufiji kwa siku mbili,(Mei 6-7, 2025) kwa lengo la kukagua utetelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ya Mwaka 2020/2025. Mkazi wa ikwiriri Bw. Abdallah Moba amesema jitihada za Mhe. Mchengerwa za kujenga barabara ya Kituo cha Afya Ikwiriri zimewawezesha wananchi kufika kwa urahisi katika kituo hicho ili kupata huduma za afya msingi. Bi. Mariam Hamza ambaye ni Mama Lishe amesema kuwa, kabla ya barabara ya Kituo cha Afya Ikwiriri kujengwa wateja wake walikuwa wakikabiliwa na changamoto ya vumbi p...

Waziri Mavunde: Mgodi Wa Magambazi Wilayani Handeni Kuanza Kazi Julai 2025

  ◾️ Kampuni ya kuendeleza mgodi kupatikana mwezi wa 5 mwishoni ◾️ Wananchi wamshukuru Rais Samia kwa kusimamia kuanza tena kwa shughuli za Mgodi Magambazi ▪️Wilaya ya Handeni kuongeza mapato zaidi ▪️Waziri Mavunde asisitiza ajira kwa wananchi wanaouzunguka Mgodi 📍Handeni, Tanga Waziri wa Madini, Mhe. Anthony Mavunde, ameeleza kuwa Mgodi wa Kati wa Dhahabu wa Magambazi uliopo Wilayani Handeni Mkoani Tanga utaanza kufanya kazi rasmi ifikapo Julai 2025 na unatarajiwa kuleta tija kwa kuchochea maendeleo ya kiuchumi na kijamii katika Kijiji cha Nyasa na Wilaya ya Handeni kwa ujumla. Waziri Mavunde ameeleza hayo leo Mei 10, 2025, wakati akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Nyasa, Kata ya Kang’ata, Wilaya ya Handeni, ambapo amekuja kuleta mrejesho wa ahadi aliyotoa Aprili 6, 2025 kuhusu hatma ya uendelezaji wa mgodi huo uliosubiriwa kwa muda mrefu. “Tunamshukuru sana Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa maelekezo yake kuhakikisha Mgodi huu wa Magambazi u...

Wanachama wa Yanga Tawi la Musoma Wachaguana Kuziba Nafasi

Na Shomari Binda-Musoma  WANACHAMA wa timu ya Yanga tawi la Musoma wamechaguana kuziba nafasi za uongozi zilizokuwa wazi. Uchaguzi huo umefanyika leo mei 10,2025 kwenye ukumbi wa Dreem Garden Resort huku viongozi waliochaguliwa wakiahidi kuendelea kuimalisha tawi hilo. Nafasi zilizozibwa kwenye uchaguzi huo ni Makamu Mwenyekiti,Mjumbe wa Mkutano Mkuu Taifa,Mweka Hazina pamoja na mhamasishaji. Akizungumza baada ya kuchaguliwa kwa nafasi ya Makamu Mwenyekiti,Cleopa Kivuyo amewashukuru wanachama wa timu hiyo tawi la Musoma kwa kumuamini na kumchagua. Amesema atashirikiana na Mwenyekiti Ismail Massaro na wanachama wote kuhakikisha wanatekeleza majukumu yote ya tawi hilo kwa mujibu wa Katiba na utaratibu. Kwa upande wake Melvin Nashon Otieno"Shuku"aliyechaguliwa kwa nafasi ya Mweka Hazina amesema kwa nafasi yake atahakikisha kila kinachotakiwa kutunzwa kwa nafasi yake kinatunzwa. Amesema kila mwanachama atakaposhiriki kwenye mchango wowote awe na imani kuwa itakuwa mikono salama n...

Dkt. Biteko Ashiriki Tulia Marathon Mbeya

📌 Ampongeza Dkt. Tulia kwa ubunifu na kusaidia wahitaji 📌 Wananchi 9,000 wapata bima za afya kupitia Tulia Marathon 📌 Awashukuru wadau na wasanii kwa kushiriki Tulia Marathon Na Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amempongeza  Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani, Mhe. Dkt. Tulia Ackson kwa mchango wake katika sekta za afya na elimu sambamba na kusaidia wahitaji jijini Mbeya. Dkt. Biteko ametoa pongezi hizo leo Mei 10, 2025 jijini Mbeya mara baada ya kukimbia mbio fupi za Tulia (Tulia Marathon) katika Uwanja wa Sokoine. “ Dkt. Tulia anafanya kazi kubwa kwenye sekta ya afya na elimu pamoja na kuwajengea nyumba watu wenye uhitaji. Zile nyumba tunazoziona anawakabidhi watu kumbe tayari kuna nyingine zimejengwa Uyole,” amesema Dkt. Biteko. Amesisitiza “ Nataka niwaambie hakuna  sadaka kubwa kama kusaidia wahitaji na sisi wengine tunajifunza kupitia wewe Dkt...

Kapinga Azindua Kituo Mama Cha Gesi Asilia Iliyoshindiliwa (Cng) Jijini Dar Es Salaam

📌 *Ni cha Pili kwa ukubwa barani Afrika; Cha Kwanza kwa ukubwa EAC* 📌 *Kujaza Gesi Asilia kwenye magari 1200 kwa siku* 📌 *Ampongeza Dkt. Samia kutatua changamoto za wananchi kwa vitendo* 📌 *Aipongeza TPDC; Ataka Vituo vya CNG kuendelea kujengwa* Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Judith Kapinga amezindua Kituo Mama cha Gesi Asilia iliyoshindiliwa (CNG) ambacho kina uwezo wa kujaza Gesi Asilia kwenye magari 1200 kwa siku huku kikifanya kazi kwa muda wa saa 24.  Kapinga amezindua kituo hicho tarehe 9 Mei, 2025 jijini Dar es Salaam akimwakilisha Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko ambapo uzinduzi huo ulienda sambamba na uzinduzi wa basi la mfano la Kampuni ya Mabasi Yaendayo Haraka (UDART) ambalo litaendeshwa kwa kutumia nishati ya Gesi Asilia. Akizungumza na halaiki iliyohudhuria hafla hiyo, Kapinga amemshukuru Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa maono, mtazamo na maelekezo yake kwa Wizara ya Nishati ambayo yanaleta matokeo chanya kielelezo mojawapo kikiwa ni ...

Wananchi Tarime Wamtaja Kembaki Kama Mbunge Wa Pekee Wakipokea Madawati

Na Shomari Binda-Tarime WANANCHI wa jimbo la Tarime mjini wamemtaja mbunge wa jimbo hilo Michael Kembaki kama mbunge wa pekee katika maendeleo ya elimu. Licha ya wananchi kumtaja mbunge huyo kama wa pekee Chama cha Mapinduzi ( CCM) Wilaya ya Tarime haikuwa mbali na wananchi hao kwa kudai ametekeleza ilani pasipo shaka. Hayo wameyasema kwa nyakati tofauti wakati wakipokea madawati yaliyotolewa na mbunge huyo kwaajili ya shule za msingi. Mmoja wa wananchi hao aliyeshuhudia upokeaji wa madawati hayo Mwita Mniko amesema wamepita wabunge kwenye jimbo la Tarime mjini kwenye sekta ya elimu Kembaki amekuwa suruhisho. Amesema madawati aliyoyatoa yanakwenda kuwafanya wanafunzi kukaa mahala sahihi pa kuwawezesha kusoma pasipo kukaa chini. Mwita amesema mbunge huyo ni mdau mkubwa wa elimu na mchango wake unaonekana kwa macho namna anavyosaidia kuinua elimu. " Tunamshukuru sana mheshimiwa mbunge kwa mchango wake wa kutoa madawati kwaajili ya shule zetu za msingi kwa lengo la kufanya kila mtoto...