Wanachama wa Yanga Tawi la Musoma Wachaguana Kuziba Nafasi

GEORGE MARATO TV
0


Na Shomari Binda-Musoma 

WANACHAMA wa timu ya Yanga tawi la Musoma wamechaguana kuziba nafasi za uongozi zilizokuwa wazi.

Uchaguzi huo umefanyika leo mei 10,2025 kwenye ukumbi wa Dreem Garden Resort huku viongozi waliochaguliwa wakiahidi kuendelea kuimalisha tawi hilo.

Nafasi zilizozibwa kwenye uchaguzi huo ni Makamu Mwenyekiti,Mjumbe wa Mkutano Mkuu Taifa,Mweka Hazina pamoja na mhamasishaji.

Akizungumza baada ya kuchaguliwa kwa nafasi ya Makamu Mwenyekiti,Cleopa Kivuyo amewashukuru wanachama wa timu hiyo tawi la Musoma kwa kumuamini na kumchagua.

Amesema atashirikiana na Mwenyekiti Ismail Massaro na wanachama wote kuhakikisha wanatekeleza majukumu yote ya tawi hilo kwa mujibu wa Katiba na utaratibu.

Kwa upande wake Melvin Nashon Otieno"Shuku"aliyechaguliwa kwa nafasi ya Mweka Hazina amesema kwa nafasi yake atahakikisha kila kinachotakiwa kutunzwa kwa nafasi yake kinatunzwa.

Amesema kila mwanachama atakaposhiriki kwenye mchango wowote awe na imani kuwa itakuwa mikono salama na kusimamiwa kutokana na lengo litakalokuwa limekusudiwa.

Naye Ally Washokera aliyechaguliwa kwa nafasi ya Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Taifa amesema atawakilisha vyema mikutano ya kitaifa pale atakaposhiriki kwa kupeleka mawazo watakayoyatoa

Pia mkutano huo wa uchaguzi mdogo umemchagua Aretus Benda kuwa mhamasishaji wa tawi hilo pamoja na Bakari Mashauri Ebambo.






Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top