Skip to main content

Posts

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Ajabu Kituo cha Polisi Kikifungwa Kwa Kushindwa Kulipa Kodi

KITUO cha polisi cha Riandira Kaunti ya Kirinyaga Nchini Kenya kimefungwa kwa muda usiojulikana kutokana na malimbikizo ya kodi Sh2 milioni. Kituo hicho kimekuwa kikiwahudumia wakazi kwa takriban miaka tisa katika jengo la kibinafsi. Kufungwa kwa kituo hicho muhimu mnamo Machi 24, kuliwafanya wakazi wa soko la Riandira na viunga vyake kuwa na hofu. Polisi walionekana wakibeba virago vyao na kuondoka, jambo lililowashangaza wakazi hao. “Maafisa hao wameondoka na hatujui walikokwenda, kwa kweli waliimarisha usalama katika eneo hili na tutateseka,” mmoja wa wakazi Bi Grace Wanjiru alisema. Mnamo 2016, Tajiri wa eneo hilo, marehemu Mwangi Thuita alitenga jengo hilo kwa polisi kuanzisha kituo cha polisi kufuatia kuongezeka kwa visa vya ukosefu wa usalama katika eneo hilo. Polisi walipaswa kuendelea kulipa kodi na kuondoka katika jengo hilo baada ya serikali kujenga kituo chake cha polisi katika eneo hilo. Hata hivyo, serikali haijaweza kujenga kituo chake cha polisi na maafisa wake wa usala...

Mchengerwa Atoa Miezi Miwili Barabara za Tarura Ikwiriri Zikamilike

OR-TAMISEMI Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mhe. Mohamed Mchengerwa, amemtaka Meneja wa Wakala wa Barabara Mijini na Vijijini (TARURA) Mkoa wa Pwani, Mhandisi Leopold Runji, kuhakikisha wakandarasi wanakamilisha ujenzi wa barabara za lami Ikwiriri ndani ya miezi miwili ili wananchi wanufaike na maboresho ya miundombinu hiyo yanayofanywa na Serikali ya Awamu ya Sita.  Mhe. Mchengerwa ametoa maelekezo hayo wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa barabara hizo wilayani Rufiji. Nao, Baadhi ya wananchi, akiwamo Dereva wa bodaboda Ramadhan Mwipi na Mama Lishe Mariam Hamza, wamemshukuru Waziri Mchengerwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuboresha barabara hiyo, wakieleza kuwa imeleta ahueni kubwa kwa usafiri na biashara zao.  "Natoa miezi miwili tu, barabara ziwe zimekamilika ifikapo Mei 30, 2025, ikiwa ni pamoja na mitaro na taa za barabarani. Hakutakuwa na nyongeza ya muda," amesisitiza Waziri Mchengerwa. Ameagiza Meneja wa TARURA kuwasimamia w...

Waziri Mavunde Aongoza Kikao cha Watendaji wa Wizara

  Waziri wa Madini Mhe. Anthony Mavunde akiongoza kikao cha Menejimenti ya Wizara na Taasisi zake ikiwa ni maandalizi ya kuwasilisha taarifa ya utekelezaji wa bajeti ya Wizara kwa Mwaka wa Fedha 2024/25 kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini. Taarifa hiyo inawasilishwa leo Machi 25, 2025.

Waziri Mkuu Azindua Lango a Utalii Hifadhi ya Mkomazi

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa leo Machi 25, 2025 amezindua lango la kuingia na kutoka watalii la Ndea kwenye Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi iliyoko Wilaya ya Mwanga Mkoani Kilimanjaro. Uzinduzi wa lango hilo ambalo limegharimu Shilingi Milioni 350 ni sehemu ya maboresho makubwa yaliyofanywa na Serikali ya Awamu ya Sita ili kuchochea na kuongeza vivutio vya utalii nchini. Akitoa taarifa ya lango hilo Mhifadhi Mkuu Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi, Emmanuel Mwailama amesema ujenzi wa lango hilo utaongeza idadi ya watalii katika mbuga hiyo ambao wengi wanakwenda kuona maisha ya wanyama pembezoni mwa ziwa jipe, Faru weusi pamoja na tembo.

Waziri Simbachawene : Watendaji Wakuu wa Serikali Acheni Kuwaona Wakaguzi wa Ndani Kama Maadui

Na. Lusungu Helela - MWANZA  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.George Simbachawene amewataka  Watendaji Wakuu pamoja na Bodi ya Wakurugenzi  kuacha kuwachukulia Wakaguzi wa Ndani  kama maadui badala yake wawape ushirikiano ili Taasisi zao zisipate  hati chafu. Amesema kumekuwa na kasumba iliyojengeka kwa Watendaji wengi wa Serikali ya kuwaona Wakaguzi hao wa Ndani kama sio Watumishi na wapo pale kwa ajili ya kuharibu mipango yao ilhali wao ni watu muhimu na jicho la Taasisi. Mhe.Simbachawene ametoa kauli hiyo leo Machi 24, 2025 jijini Mwanza wakati akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt.Samia Suluhu Hassan kufungua Mkutano wa tatu wa Wakaguzi wa Ndani wa Sekta ya Umma.  Amesema Mtendaji  yeyote wa Serikali  anayewatumia vizuri Wakaguzi wa Ndani hawezi kuingia kwenye matatizo ya ubadhirifu wa fedha za umma huku akisisitiza kuwa Wakaguzi hao wapo kwa ajili ya kumsaidia yeye na...

Rais Samia Ashiriki Mkutano wa Pamoja na Wakuu wa Nchi wa Eac na Sadc Kwa Njia ya Mtandao

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akishiriki Mkutano wa Pamoja wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) uliofanyika kwa njia ya mtandao tarehe 24 Machi, 2025 Ikulu ndogo ya Mkanyageni, Chake Chake, mkoa wa Kusini Pemba. Mkutano huu ni wa pili kufanyika baada ya ule wa kwanza uliofanyika tarehe 08 Februari, 2025 Ikulu, Jijini Dar es Salaam na ulihudhuriwa na Wakuu wa Nchi na Serikali wafuatao:- Rais William Ruto wa Kenya, Dkt. Emmerson Mnangagwa wa Zimbabwe, Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini, Rais Yoweri Museveni wa Uganda, Rais Paul Kagame wa Rwanda, Rais Lazarus Chakwera wa Malawi, Rais Andry Rajoelina wa Madagascar, Rais Hakainde Hichilema wa Zambia, Dkt. Samia Suluhu Hassan wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Waziri Mkuu wa Somalia pamoja na Mawaziri kutoka Sudani Kusini na Angola.