Skip to main content

Posts

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Naibu Waziri Mkuu Kuzindua Mpango Kazi wa Watu Wenye Ualbino

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko akiwasili katika ukumbi wa Diamond Jubilee - Dar es Salaam, kuzindua Mpango Kazi wa Taifa wa Haki na Ustawi wa watu wenye Ualbino pamoja na mkakati wa Taifa wa Teknolojia Saidizi unaolenga kuongeza ufahamu wa changamoto za watu wenye ulemavu. Mikakati hiyo inazinduliwa leo Disemba 03, 2024 ambayo pia ni Siku ya Kimataifa ya Watu wenye Ulemavu ambayo Kauli mbiu yake ni 'Kukuza uongozi wa watu wenye ulemavu kwa ajili ya mustakabali jumuishi na endelevu'. 

Waziri Mkuu ashiriki maziko ya Dkt.Ndugulile

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Desemba 03, 2024 ameshiriki mazishi ya aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Kigamboni na Mkurugenzi Mteule wa Shirika la Afya Duniani Kanda ya Afrika, Dkt. Faustine Ndugulile yaliyofanyika eneo la Mwongozo, Kigamboni Jijini Dar es Salaam. Viongozi wengine walioshiriki Mazishi hayo ni Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu William Lukuvi, Waziri wa Afya Jenista Mhagama, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila na viongozi wa Chama na Serikali. Dkt. Ndugulile alifariki usiku wa kuamkia Novemba 27, 2024 nchini India ambapo alikuwa akipatiwa matibabu.

Mhandisi Seff awashukuru wale wote waliompigia kura tuzo za ' CEO ' bora wa mwaka 2024

#Awataka watumishi kuchapa kazi kutimiza lengo la Serikali  Dodoma Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Barabara za VIjijini na Mijini (TARURA), Mhandisi Victor Seff amewashukuru Watanzania wote waliojitokeza na kumpigia kura wakati akiwania tuzo za Mtendaji/Mkurugenzi Mkuu Bora wa mwaka 2024 kati ya Wakurugenzi 100 walioteuliwa kuwania tuzo hizo (Top 100 Executive List Awards) na yeye kuibuka kinara. Mhandisi Seff ameyasema hayo leo tarehe 3/12/2024 jijini Dodoma wakati akiongea na watumishi waTARURA Makuu mara baada ya kuwasili ofisi za Taasisi hiyo zilizopo Mji wa Serikali Mtumba. Mhandisi Seff amewashukuru watumishi wote kwa ushirikiano wao katika utendaji kazi wa Taasisi hiyo na hivyo kumfikisha hapo alipo "Hili sio jambo dogo, ni jambo la kumshukuru Mungu sana. Naomba tuendelee kumshukuru Mungu ili Taasisi yetu iendelee kufanya vizuri". Aidha, amewataka watumishi hao kuendelea kufanya kazi kwa ushirikiano ili kutimiza malengo ya Serikali pamoja na kuendeleza yale ambayo yeye amey...

Waziri Mkuu afungua Mkutano Mkuu wa Chama cha Majaji na Mahakimu

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa ametoa wito kwa Chama cha Majaji na Mahakimu wa Afrika Mashariki kuendelea kujadili changamoto katika utoaji haki na kuweka mipango endelevu ya namna ya kukabiliana na changamoto hizo kupitia mikutano yake. Ametoa wito huo leo (Disemba 03, 2024) alipomwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika mkutano wa Ishirini na Moja wa chama hicho uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa hotel ya GranMelia jijini Arusha. “Mkutano huu pamoja na mambo mengine ni muhimu kujadili masuala muhimu ya Kitaifa na Kikanda katika mfumo wa utoaji haki, pia nina imani kupitia mkutano huu mtajadili umuhimu wa kuimarisha na kuboresha mifumo ya utoaji haki na kutumia ukuaji wa teknolojia ili kuboresha kwenye ufanisi wa majukumu yenu” Pia, Mheshimiwa Majaliwa amewataka Majaji na Mahakimu hao kujadili namna mifumo ya utoaji haki inavyoweza kuwa chachu ya ushirikiano wa kikanda na ukuaji wa uchumi. “Mnapaswa kujadili namna mifumo ya utoaji haki inavyoweza kusaidia katika kukuza mtang...

Waziri Mkuu Majaliwa Kumwakilisha Rais Samia Mkutano wa Majaji na Mahakimu Afrika Mashariki

 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Disemba 03, 2024 amemwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika mkutano wa Ishirini na Moja wa Chama cha Majaji na Mahakimu wa Afrika Mashariki. Mkutano huo unafanyika katika ukumbi wa mikutano wa Hotel ya Grand Melia, jijini Arusha.

Tanapa Yapokea Mitambo na Malori Yenye Thamani ya Shilingi Billioni 6.4

Na Philipo Hassan/ Dar es salaam Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Dkt. Pindi Chana (Mb) amewakabidhi TANAPA Malori matano na mitambo mitano yenye thamani ya Dola milioni 2.4 sawa na shilingi Bilioni 6.4 za Kitanzania, tukio hilo limefanyika leo Disemba 2, 2024 katika Ukumbi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (Mpingo House) jijini Dar es salaam. Vifaa hivyo viliyonunuliwa kupitia mradi wa Dharura kwa Uhifadhi na Utalii Tanzania (Emergency Recovery Support for Biodiversity in Tanzania) kupitia benki ya Maendeleo ya Ujerumani (KFW). Akizungumza katika makabidhiano haya Balozi Dkt. Chana alieleza kuwa vifaa hivyo vitaboresha shughuli za Uhifadhi pamoja na miundombinu katika Hifadhi za Taifa Serengeti na Nyerere kwa malengo ya kupunguza athari zilizosababishwa na janga la UVIKO-19 kwenye Utalii na Uhifadhi. Dkt. Chana alisema “Nawaagiza Bodi na Wakuu wa Mashirika ya TAN