Skip to main content

Posts

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Ccm yasambaza "Bunduki na Risasi" Zake Zote Nchi Nzima

_Ni uzinduzi wa kampeni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa_   _Katibu Mkuu Balozi Nchimbi kuongoza kampeni hizo_   _Yaonesha umuhimu wa uchaguzi na dhamira ya kufikia wananchi moja kwa moja_   Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi, anatarajiwa kuzindua kampeni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa za CCM Mkoa wa Mwanza tarehe 20 Novemba 2024, akiongoza viongozi na makada wa CCM waliotumwa maeneo mbalimbali nchini kwa kazi hiyo.   Balozi Nchimbi, ambaye pia ni mlezi wa CCM Mkoa wa Mwanza, atazindua kampeni hizo katika mkutano wa hadhara utakaofanyika Uwanja wa Furahisha, Nyamagana, jijini Mwanza.   Wajumbe wa Kamati Kuu ya CCM, ambao ni walezi wa mikoa mingine, pamoja na Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC), wamepewa jukumu la kuzindua kampeni hizo katika mikoa yote 26 ya Tanzania Bara kwa tarehe hiyo hiyo.   Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara), Ndugu John Mongella, atazindua kampeni Mkoa wa M...

Rais Samia amelipa viingilio vyote kuiona stars leo kea mkapa

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan awalipia viingilio watanzania wote kwenda uwanjani na kushuhudia mchezo wa Tanzania dhidi ya Guinea unatarajia kuchezwa leo Novemba 20-2024 uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam. Mechi hiyo ya kufuzu kwa Mashindano ya Mataifa Afrika (AFCON) itachezwa leo jioni katika Uwanja huo wa Benjamin Mkapa, Jijini Dar es Salaam. Akiwasilisha taarifa hiyo, Dkt. Doto Biteko amesema Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan ameelekeza kuwa watu wote waingie uwanjani bure na hivyo wananchi wajitokeze kwa wingi kwenda kuitia moyo timu yetu ya Taifa Stars na kwakweli imefanya vizuri sana kwenye mechi iliyopita na tunaamini mechi hii tutashinda ili tuweze kusonga mbele.

Waziri Mkuu amwakilisha Rais Dkt. Samia Mkutano wa Kimataifa wa Madini na Uwekezaji 2024

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Novemba 19, 2024 amemwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika mkutano wa Kimataifa wa Madini na Uwekezaji Tanzania, kwenye kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam. Mkutano huo unawakutanisha wadau wa madini wanaojishughulisha na utafutaji, uchimbaji, uchenjuaji, uongezaji thamani madini, wasimamizi wa Sekta kutoka Serikalini, watoa huduma migodini na wafanyabiashara. Pamoja na malengo mengine, mkutano huo umelenga kuweka mipango ya kuvutia uwekezaji  wa nje ya nchi, kukuza usimamizi bora wa rasilimali za Madini pamoja na kubadilishana uzoefu na washiriki kutoka maeneo mbalimbali duniani. Kaulimbiu ya mkutano huo ni _Uongezaji wa Thamani ya Madini kwa Maendeleo ya Kiuchumi

Waziri Kombo aongoza Mkutano wa dharura wa kamati ya Mawaziri wa asasi ya siasa, ulinzi na usalama ya Sadc

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo (Mb.), ameongoza Mkutano wa Dharura wa Kamati ya Mawaziri wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini Mwa Afrika (SADC-Organ) uliofanyika tarehe 17 Novemba , 2024 jijini Harare, Zimbabwe. Waziri Kombo ameungana na Mawaziri wenzake wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kujadili hali ya usalama Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) pamoja na njia mbalimbali za kurejesha amani nchini humo. Akizungumza katika Mkutano huo, Balozi Kombo amebainisha kuwa Tanzania inaunga mkono juhudi zote zinazofanyika katika kurejesha amani Mashariki mwa DRC.  Aidha, Balozi Kombo amezisisitiza Nchi za SADC kushirikiana ili kutafuta suluhu ya kudumu ya kurejesha amani Mashariki mwa Nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC). “Ni jukumu la kila Nchi Mwanachama kushirikiana kwa pamoja katika kurejesha amani na usalama kwa nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (...

Dkt. Biteko amesema hataki kusikia visingizio kwa mashirika ya umma kushiriki kwenye michezo

*📌 Asema haiwezekani kutenga bajeti ya michezo kisha kuitumia vinginevyo* *📌 Amtaka Msajili wa Hazina kushiriki ufungaji bila kuwakilishwa* *📌 Shimmuta yashukuru kwa ushirikiano wa Serikali kuongeza wanachama* *Na Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati* Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mheshimiwa Dkt. Doto Biteko amemwakilisha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Phillip Mpango kufungua mashindano ya Shirikisho la Michezo ya Mashirika ya Umma nchini SHIMMUTA na kuagiza mashirika kuondokana na visingizio visivyo na msingi ili kutimiza azma ya mashindano hayo. Dkt. Biteko ametoa maelekezo hayo Jijini Tanga ambapo amesema kumekuwa na visingizio vya kuwakosesha watumishi wa umma kushiriki mashindano ilhali ni suala linalofahamika na liko kwenye kalenda ya kila mwaka ya mashirika husika. “Utaratibu huu wa kukubaliana jambo lakini jambo tulilokubaliana halifanyiki inatufanya tukose uhalali wa kuwasimamia wengine, nilitaka kujua kwanini hatupeleki wa...

Jwtz imeshauri iwepo Mitaala ya Mafunzo ya amani na usalama

 Mkuu wa Kamandi ya Vikosi chini ya Makao Makuu Meja Jenerali Iddi Said Nkambi amevishauri Vyombo vya Ulinzi na Usalama, Taasisi za Serikali na Kiraia zinazohusika na Ulinzi wa Amani chini ya Mwavuli wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika ( SADC) kuhakikisha zinandaa mitaala ya kuendeshea mafunzo ya Ulinzi wa Amani kwa kuzingatia matishio yanayozikabili nchi wanachama. Meja Jenerali Nkambi ameyasema hayo leo tarehe 18 Novemba 2024 wakati wa ufunguzi wa Semina fupi ya siku 5 inayohusu uwasilishaji wa mitaala mipya ya mafunzo itakayotumika kuandaa Majeshi ya SADC, semina inayofanyika katika Kituo cha Mafunzo ya Ulinzi wa Amani (PTC) kilichopo Kunduchi Jijini Dar es salaam. Semina hiyo inayoendeshwa na Chuo cha Ulinzi wa Amani cha Kikanda chenye Makao Makuu yake nchini Zimbabwe inahudhuriwa na washiriki kutoka nchi wanachama wa SADC ikiwa na lengo la kuwajengea uwezo katika kukabiliana na matishio pindi wanapokuwa katika majukumu ya Ulinzi wa Amani ndani ya ukanda wa S...