Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan awalipia viingilio watanzania wote kwenda uwanjani na kushuhudia mchezo wa Tanzania dhidi ya Guinea unatarajia kuchezwa leo Novemba 20-2024 uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
Mechi hiyo ya kufuzu kwa Mashindano ya Mataifa Afrika (AFCON) itachezwa leo jioni katika Uwanja huo wa Benjamin Mkapa, Jijini Dar es Salaam.
Akiwasilisha taarifa hiyo, Dkt. Doto Biteko amesema Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan ameelekeza kuwa watu wote waingie uwanjani bure na hivyo wananchi wajitokeze kwa wingi kwenda kuitia moyo timu yetu ya Taifa Stars na kwakweli imefanya vizuri sana kwenye mechi iliyopita na tunaamini mechi hii tutashinda ili tuweze kusonga mbele.

.jpg)