Na Richard Mrusha Geita. Mwenyekiti wa chama cha Wachimbaji wadogo Mkoa wa Geita (GEREMA) Titus Kabuo na mwekezaji katika sekta ya madini mkoani Geita Titus Kabuo ameonyesha mfano kama kiongozi kwa kuchukua hatua ya kipekee ya kuingia ndani ya maduara yenye urefu wa mita 400 chini ya ardhi kwenye migodi yake ya dhahabu. Kabuo, alichukua hatua hiyo ili kuhamasisha wafanyakazi wake kujiandikisha kwenye daftari la wapiga kura Hatua hiyo inalenga kuwapa wafanyakazi wake nafasi ya kushiriki kikamilifu katika michakato ya kidemokrasia ya nchi yao, jambo linaloweza kuleta mabadiliko chanya kwa jamii na taifa kwa ujumla. Akizungumza na waandishi wa habari alioambatana naye kwa wafanyakazi wa mgodi huo, Kabuo alisisitiza umuhimu wa kila raia kutumia haki yake ya kidemokrasia kwa kujiandikisha kupiga kura. "Sisi sote tuna wajibu wa kuhakikisha kuwa sauti zetu zinasikika katika masuala muhimu ya kitaifa, na njia pekee ya kufanya hivyo ni kwa kushiriki kikamilifu katika uchagu...
Marato tv - Sauti ya Jamii