Misungwi kuandikisha wapiga kura 232,128 katika daftari la makazi

GEORGE MARATO TV
0


Zoezi la uandikishaji wa wapiga kura katika Daftari la makazi linaendelea vyema katika Halmashauri ya wilaya Misungwi Mkoani Mwanza ambapo zaidi ya wapiga kura  elfu thelathini tayari wameandikishwa katika daftari hilo.

Afisa uchaguzi wa Halmashauri hiyo Dickson Kawovela amesema kuwa idadi hiyo ambayo ni sawa na asilimia 33 inajumuisha wanaume 33,234 pamoja na wanawake 35,291.

Akizungumza wakati wa kukagua zoezi la uandikishaji katika kata ya misungwi,Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya misungwi,Addo Missama amesema kuwa mwelekeo ni mzuri na matarajio ni kufikia malengo ya kuandikisha watu 232,128.

Missama amewaasa wananchi ambao hawajajiandikisha kutumia siku zilizosalia kujiandikisha ili waweze kuchagua viongozi wanaowataka katika uchaguzi wa serikali za mitaa ambao umepangwa novemba 27 mwaka huu.

‘’Nahamasisha kila mmoja kutumia haki yake kuanzia zoezi lilipoanza oktoba 11 hadi 20 mwaka huu kuweza kujiandikisha na waweze kuwa katika nafasi ya kupiga kura na kuchagua viongozi wanaowataka’’alisema Missama.

Baadhi ya wakazi wa Misungwi ambao wamejiandikisha wamesema kuwa wanasubiri novemba 27 na wako tayari kujitokeza kuchagua viongozi wanaowataka.

Wakazi hao Joyce Philipo,Salum Abdulkarim na Penda Kapera wa vitongoji vya Majengo na Old Misungwi Mjini Misungwi wametoa wito kwa wananchi ambao hawajajiandikisha kutumia siku zilizosalia kujiandikisha ili kutopoteza haki yao ya kuchagua viongozi wanaowataka.







 

 


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top