Skip to main content

Posts

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Serikali kutoa fedha za kuendeleza ujenzi wa veta rorya

  Naibu Waziri Wizara ya  Elimu, Sayansi na Teknolojia Omary Kipanga ametembelea na kukagua ujenzi wa chuo cha VETA Rorya Mkoani Mara.  Ujenzi wa majengo ya chuo hicho umefikia kwenye hatua mbalimbali. Akizungumza wakati wa ukaguzi huo, Kipanga amewahakikishia wakandarasi na wananchi wa Rorya kuwa Mhe. Dr. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania atatoa fedha mwanzoni mwa mwezi Oktoba 2024 ili shughuli za ujenzi ziiendelee.  Naye Mkuu wa Wilaya  Rorya Mhe. Dkt. Khalfan Haule amemshukuru Naibu waziri kwa kutembelea na kujionea changamoto za ujenzi wa mradi huo. Amemwomba Naibu waziri Kipanga amfikishie salaam za shukrani Rais wetu mpendwa kwa kutoa fedha za kuendelea na ujenzi ili chuo hiki kiweze kutoa huduma ya mafunzo kwa vijana wa Rorya.

Rais samia azindua soko la madini ya vito na dhahabu tunduru

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amezindua Soko la Madini ya Vito na Dhahabu Wilayani Tunduru ikiwa ni moja ya shughuli alizofanya akiwa katika ziara ya kikazi ya siku 6 Mkoani Ruvuma. "Kwa dhati kabisa, napenda kuipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru kwa utekelezaji wa Sera ya kushirikiana na sekta binafsi yaani Public Private Partnership kwa vitendo ambapo Serikali imeweka fedha kiasi na kiasi kingine kimechangiwa na wafanyabiashara wa madini waliopo hapa  Wilayani Tunduru" "Ni dhahiri kwamba ujenzi wa soko hili kubwa na la kisasa utarahisisha biashara ya madini Wilayani hapa na kuongeza ufanisi katika ukusanyaji maduhuli ya Serikali sambamba na kudhibiti udanganyifu na utoroshaji wa madini", alibainisha Mhe. Rais. Aidha, Rais Samia ameonesha wazi kufurahishwa na ushirikiano huo wa Halmashauri na Sekta binafsi na kusisitiza kwamba Sera ya PPP ikitelezwa kwa vitendo ni chachu ya maendeleo ya wananchi katika Wilaya zote nchini. Pi...

Mtandao wa kutokomeza ndoa za utotoni Tecmn wafanya ziara shinyanga

Na Elizabeth Cornely,SHINYANGA Wadau kutoka mashirika ya Kutokomeza Ndoa za Utotoni Tanzania(TECMN), umetembelea kituo kinachofanya kazi ya kuokoa, kulea na kuwaendeleza watoto wa kike ambao wamekumbwa na madhila ya ukatili na kukatisha masomo kwa mimba na ndoa za utotoni kilichopo katika Kata ya Chibe wilaya ya Shinyanga mkoani Shinyanga. Wadau kutoka katika mashirika hayo zaidi 80 wamewakilishwa na machache kutoka Msichana Initiative, Medea, Plan International, My Lagacy, Binti Makini Foundation na Theatre Arts Feminist Group, ikiwa ni sehemu ya ziara yao wanayoifanya katika mikoa minne ya Mara, Shinyanga, Tabora na Dodoma. Mratibu wa Mtandao huo, Lilian Kimati, anasema wameamua kutembelea kituo hicho ili kusikiliza na kushuhudia maisha wanayoishi mabinti hao waliokumbwa na madhila ya ukatili na kuona namna ya kutoa mchango wao. Mlezi wa kituo hicho kinachojulikana kama Agape Knolwedge Open School, anasema kwa mwaka anapokea wasichana zaidi ya 50 waliopata mimba za utotoni na wale ...

Rais Samia aondoa giza jimbo la prof.Muhongo

Na Shomari Binda-Musoma MKUU wa Wilaya ya Musoma Juma Chikoka amemshukuru Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuling'arisha jimbo la Musoma vijijini kwa mwanga wa taa za barabarani. Shukrani hizo amezitoa jana septemba 25 mara baada ya kukitembelea usiku Kijiji cha Suguti kilichopo kwenye jimbo hilo. Amesema kufungwa na kuwashwa taa za barabarani kumewezesha wananchi kuendelea kufanya shughuli zao za kiuchumi hadi usiku. Amesema Rais Dkt.Samia ameendelea kufanya kazi kubwa katika kuhakikisha wananchi mjini na vijijini wanafanya shughuli za kiuchumi mchana na usiku kwa usalama. Chikoka amesema wananchi wa Kata na Kijiji cha Suguti wameonyesha furaha kwa kupata mwanga wa taa barabarani na kufanya biashara hadi usiku. Mkuu huyo wa Wilaya amesema hilo ni jambo kubwa lililofanywa na Rais Dkt.Samia na sio la kuacha kushukuru. " Hapa sio daraja la Tanzanite jijini Dar es salam bali ni Kijiji cha Suguti jimbo la Musoma vijijini limeng'aa na kuwaka. " Sasa wananchi wanafanya shug...

Serikali yakubali ombi la mbunge Mathayo kupandisha hadhi chuo cha veta musoma

 Na Shomari Binda-Musoma SERIKALI kupitia Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia imekubali ombi la mbunge wa jimbo la Musoma mjini Vedastus Mathayo kupandisha chuo cha ufundi Veta Musoma. Ombi la mbunge Mathayo alilitoa bungeni alipouliza swali ni lini Waziri wa Wizara hiyo angefika Musoma na kukitembelea chuo hicho kwaajili ya kukiona chuo hicho na kuona uhitaji wake ili kukipandisha hadhi. Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Juma Omary Kipanga kwa niaba ya Waziri wa Wizara hiyo Profesa Adolf Mkenda leo septemba 26 amekitembelea chuo hicho. Akizungumza chuoni hapo Naibu Waziri huyo amesema wametekeleza ombi la mbunge Mathayo ya kufika chuoni hapo na kupata taarifa juu ya chuo hicho. Amesema taarifa imeeleza mahitaji yanayohitajika kuwepo chuoni hapo ili kukipandisha hadhi na kutoa maelekezo ili yaweze kutekelezwa. Kipanga amesema moja ya mahitaji ni kuongezwa kwa kozi kutoka 9 na kufikia 10 pamoja na kuongezwa kwa madarasa,mabweni,eneo la kupata chakula,jiko pamoja na kalak...

Mradi wa utafiti wa simba chachu ya utalii serengeti

Taarifa za kisayansi  zinazotokana na Mradi wa muda mrefu wa Utafiti  wa SIMBA SERENGETI unaoratibiwa na Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania (TAWIRI) kupitia  Kituo cha Utafiti wa Wanyamapori Serengeti, zimekua chachu katika uhifadhi  na kivutio   cha Utalii  ndani ya hifadhi  ya  Taifa  Serengeti. Mradi huu wa SIMBA SERENGETI unafuatilia   idadi, tabia na mienendo ya makundi ya simba kwa zaidi ya miaka 50, ambapo kwa sasa yapo makundi 20 yenye jumla ya simba takribani 300 yanayofuatiliwa. Aidha, Katika mradi  wa SIMBA  SERENGETI utambulisho hufanyika  kwa kila Simba kuandaliwa kadi maalumu  (Lion  identification  card) kwa kutumia alama/madoa ya Kipekee  kwenye  uso eneo la ndevu (Whisker spots) na  alama nyinginezo za asili.Utambulisho huu husaidia kumfuatilia simba mmoja mmoja ndani ya kundi. Aidha matumizi ya teknolojia  yanarahisisha utafiti wa simba ambapo  kwa...