Naibu Waziri Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Omary Kipanga ametembelea na kukagua ujenzi wa chuo cha VETA Rorya Mkoani Mara.
Ujenzi wa majengo ya chuo hicho umefikia kwenye hatua mbalimbali.
Akizungumza wakati wa ukaguzi huo, Kipanga amewahakikishia wakandarasi na wananchi wa Rorya kuwa Mhe. Dr. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania atatoa fedha mwanzoni mwa mwezi Oktoba 2024 ili shughuli za ujenzi ziiendelee.
Naye Mkuu wa Wilaya Rorya Mhe. Dkt. Khalfan Haule amemshukuru Naibu waziri kwa kutembelea na kujionea changamoto za ujenzi wa mradi huo.
Amemwomba Naibu waziri Kipanga amfikishie salaam za shukrani Rais wetu mpendwa kwa kutoa fedha za kuendelea na ujenzi ili chuo hiki kiweze kutoa huduma ya mafunzo kwa vijana wa Rorya.