Mawaziri wa ulinzi wa nchi za Tanzania na Mzumbiji wamesaini mikataba ya makubaliano ya kulinda usalama baina ya nchi hizo mbili, mawaziri hao masesaini makubaliano hayo wakati wa ufungaji wa Mkutano wa tume ya pamoja ya kudumu ya ulinzi na usalama kati ya Tanzania na Msumbiji kilichofanyika katika ukumbi wa The Aga Khani Diamond jubilee jijini Dar es Salaam.
Akizungumza baada ya mkutano huo Mkuu wa kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Luteni Kanali Kelvin Baraka Byabato amesema madhumini makuu ya kikao hicho ni kuendeleza maono ya waasisi wa mataifa haya hayati mwalimu Julius Nyerere na Samora Masheli wa Msumbiji.
Mkutano huu wa siku nne ni mwendelezo wa Mikutano ya awali ambao huu ni Mkutano wa saba kufanyika huku kikao cha nane kikitarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwaka 2027 Jijini Maputo nchini Msumbiji.






Comments
Post a Comment