Na Mwanamkuu Mwandoro, Tanga.
Mkuu wa mkoa wa Tanga Balozi Dkt. Batilda Burian amewashukuru wanawake wote wa mkoa huu waliojitokeza katika Dua maalum ya kuwaombea aliyekuwa mume Rais Samia Suluhu Hassan Marhum Hafidh Ameir na aliyekuwa mke wa Rais wa kwanza wa Zanzibar Marhumat Bi. Fatma Karume iliyofanyika katika ukumbi wa Simba Mtoto jijini hapa.
Aidha Balozi Batilda amesema aliamua kufanya hivyo kwani ulipotokea msiba wa mume wa Rais yeye alikuwa nje ya nchi na hakupata nafsi ya kuhudhiria hivyo basi aliona hiyo ndio njia pekee ya kumuenzi Marhum huyo na kufuatia msiba ma bi. Fatma Karume akaona afanye Dua hiyo ya pamoja.
"Niwashukuru sana JUWAKITA kwa kuniunga mkono katika jambo hili la kheri kwani sikutegemea,maandalizi yalikuwa ya muda mfupi pamoja na kuchelewa kuwapa taarifa lakini muitikio wenu umenifinza kitu kikubwa,Sina cha kuwalipa Allah ndiye atawalipa", mesema Balozi Batilda.
Nao Jumuiya Ya Wanawake Wa Kiislam Tanzania (JUWAKITA) Tanga wamempongeza mkuu huyo wa mkoa kwa alicho kifanya kwani mtu anapofariki chakula chake kikuu hubaki kuwa Dua.
Akizungumza baada ya kisomo hicho maalum Mwenyekiti wa JUWAKITA Mkoa wa Tanga Bi.Sophia Uledi amesema mkuu wa mkoa amefanya jambo zuri na anastahili pongezi na kuigwa na wengine.




Comments
Post a Comment