Na Mwanamkuu Mwandoro, Tanga.
WANANCHI wa mkoa wa mkoa wa Tanga wametakiwa kufuata Sheria,kanuni na Sheria mdogo za usafi wa mazingira zinazowataka kuhakikisha maeneo yanayo wazunguka yanakuwa safi na kutotupa taka ovyo.
Hayo yamesemwa na mkuu wa mkoa huo Balozi Dkt. Batilda Burian baada ya uzinduzi wa "Dkt. Batilda Mazingira Day" siku yenye kuhamasisha usafi iliyoungwa mkono na viongozi mbalimbali akiwemo Mkuu wa Wilaya,Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga,katibu Tawala wa mkoa na wengineo.
Aidha mpango huo unakusudiwa kuhakikisha usafi wa mazingira unakuwa endelevu kwa Kila mwananchi sambamba na kuimarisha ulinzi,kuendelea kutoa elimu Kwa wananchi na utekelezaji wa Sheria katika maeneo ya makazi,biashara,masoko,na maeneo ya wazi.
Pamoja na hayo Dkt. Batilda amesema yeyote atakae kamatwa akitupa taka hovyo atachukuliwa hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na kutozwa faini na faini ya chini kabisa ni kiasi cha shilingi elfu hamsini na malipo ya faini yatafanyika kupitia mfumo rasmi na sio kwa fedha saslim.
Nae Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga Mhe. Mustafa Mhina "Seleboss"amesema zoezi hilo litakuwa endelevu na kutilia mkazo maagizo yaliyotolewa na mkuu wa mkoa kuanza mara moja utekelezaji wake.
Dkt. Batilda Mazingira Day inakauli mbiu isemayo "MTAA SAFI,KATA SAFI JIJI SAFI TIANZE LEO", na zoezi hili la usafi litakiluwa likifanyika kila jumamosi ya kwanza wa mwezi.




Comments
Post a Comment