ZANZIBAR MAGAZINE YAZINDULIWA NEW YORK, YAANGAZIA MAONO YA MAMA MARIAM MWINYI KATIKA UCHUMI WA BULUU
Jarida la Zanzibar Magazine limezinduliwa pembezoni mwa Mkutano wa 81 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UNGA 81), jijini New York, Septemba 2026 likiwa na makala maalum inayoangazia kazi zinazofanywa na Zanzibar Maisha Bora Foundation (ZMBF) pamoja na maono ya Mama Mariam Mwinyi katika kuendeleza Uchumi wa Buluu Zanzibar.
Makala hiyo, inayoanzia ukurasa wa 12, inaangazia umuhimu wa kuwa na mtazamo shirikishi na jumuishi katika kurndeleza Uchumi wa Buluu, hususan katika sekta ya kilimo cha mwani, kwa kuzingatia nafasi na mchango wa wanawake na vijana.
Aidha, makala hiyo inaeleza juhudi zinazofanywa na Serikali pamoja na wadau mbalimbali katika kuwawezesha wanawake na vijana kunufaika na fursa za Uchumi wa Buluu, na kuibadilisha shughuli ya kilimo cha mwani kutoka uzalishaji wa kujikimu na kuwa shughuli endelevu na yenye tija kiuchumi.
Uzinduzi wa jarida hilo unaendelea kutoa fursa ya kuonesha juhudi, mafanikio na fursa zilizopo Zanzibar katika kuwawezesha wananchi, hususan wanawake na vijana, kushiriki kikamilifu katika maendeleo ya Uchumi wa Buluu.


Comments
Post a Comment