Na Mwandishi wetu Jovina Massano.
Makamu Mwenyekiti Wa chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) John Wegesa Heche amesema kuwatoza ushuru mara mbili wachuuzi wa dagaa Manispaa ya Musoma ni kuwaumiza.
Amesema hayo kwenye mkutano wa hadhara wakati akihutubia wananchi katika viwanja vya Shule ya sekondari Mara Septemba 25,2026.
Kauli hiyo ameitoa mara baada ya Mwenyekiti CHADEMA Wilaya ya Musoma Urasa Jackson kuelezea changamoto zilizopo upande wa wajasiriamali wa dagaa.
Heche amesema kuwatoza ushuru mara mbili ni kuwaumiza wachuuzi kwa kuwa vipato vyao ni vidogo watawezaje kumudu ghalama za maisha na kuziendesha familia zao.
" Nchi hii ina madini mengi ambayo yanaweza kuchangia fedha nyingi kupitia tozo mbalimbali kwa nini wawaumize wauza dagaa wenye biashara ndogo huu ni uonevu ,"amesema Heche.
Urasa amesema kuwa wachuuzi hutozwa ushuru wa Dagaa ndoo ya lita 20 hulipia Shillingi 1000 kwa mwezi 30,000/= ambapo kwa Mwaka ni 360,000/=na ya lita 10 wanalipia shillingi 500 kwa mwezi 15,000/= kwa mwaka ni 180,000/= hivyo amemwomba makamu Mwenyekiti CHADEMA Taifa awasemee wachuuzi hao.
Nae Mtunza hazina wa CHADEMA Kanda ya Serengeti Rucy Siprian ameongeza kuwa tozo hiyo si kwa mwaroni pekee bali hata zikishakauka na kupelekwa sokoni hutozwa ushuru pia kwa hiyo tozo kwa mchuuzi wa dagaa ni zaidi ya mara moja.




Comments
Post a Comment