Na Mwanamkuu Mwandoro, Tanga.
WANANCHI nchini wametakiwa kuitazama Bahari kwa jicho la tatu kwani ikitumika vizuri inaweza kuikwamua jamii kubwa kiuchumi kwani inafursa nyingi za kibiashara zinaendeela kufunguka kutokana na maendeleo yanayofanywa na Serikali.
Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Mammlaka ya usafiri Baharini Zanzibar Sultan Said Suleiman wakati akizungumza kwenye Maadhimisho ya siku ya uzinduzi wa siku ya usafiri majini Duniani yanayoendelea kufanyika mkoani Tanga.
Kwa Upande wake mkurungenzi mkuu wa Bodi ya Mamlaka ya Usafiri Majini Zanzibar (ZMA) Akif Ally Khamis amesema maboresho ya baadhi ya Bandari ikiwemo bandari ya Tanga,Marhubi, pamoja na Kizimkazi yanatajwa kuwa chachu ya maendeleo katika sekta ya usafirishaji na biashara na ndani na nje ya nchi.
Aidha Akif amesema hali ya kibiashara imepanuka zaidi Kwa sasa tofauti na awali ambapo shehena za mizigo zimeongezeka ikiwemo mizigo ya saruji pamoja na vyakula na vyote hivyo husafirishwa kupitia bandari zetu.

Comments
Post a Comment