Skip to main content

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

PART TWO: KATIBA YASEMA NINI? SERIKALI NI NINI, VYOMBO VYA DOLA NI VYA NANI - WACHAMBUZI WAENDELEA KUMUUNGA MKONO COMRADE CHACHA


 

Na Mwandishi Wetu Maalum

Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya 1977 ndio inaojibu kila kitu kuhusu kauli iliyotolewa na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Idara ya Oganaizesheni, Ndugu Paul Chacha, aliposema hadharani kuwa Chama Cha Mapinduzi ndicho mmiliki halali wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Jeshi la Polisi na Idara ya Usalama wa Taifa, na kuwa viongozi wote wa Serikali wamewekwa na CCM na sio na wananchi kama wengi wanavyodhani.

Kauli hiyo imeibua mjadala mkali mitandaoni ambapo wapinzani wamejaribu kuipotosha kama ni kauli ya kichochezi. Lakini uchambuzi wa kina wa Katiba na misingi ya Sayansi ya Siasa unaonyesha kuwa Ndugu Chacha yupo sahihi kwa asilimia mia moja.

Katiba yenyewe ndio inathibitisha hilo. Ibara ya 4 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano inasema kwa maneno yasiyopindika kuwa Jamhuri ya Muungano ni nchi ya kidemokrasia na ya kijamaa inayofuata mfumo wa vyama vingi, na kwamba mamlaka yote ya dola yatatumika na kudhibitiwa na vyombo vitatu tu ambavyo ni Bunge, Mahakama na Serikali.

Lakini swali la msingi ambalo wananchi wengi hawaliulizi ni je, Serikali ni nini na inatoka wapi? Jibu lipo kwenye Katiba hiyo hiyo. Serikali haipo angani. Serikali inazaliwa na chama cha siasa kilichoshinda uchaguzi mkuu. Bila chama cha siasa hakuna Serikali. Na bila Serikali hakuna vyombo vya dola. Hivyo anayezalisha Serikali ndiye mmiliki wa vyombo vya dola.

Ibara ya 147(1) ya Katiba ya Jamhuri inasema wazi kabisa bila kuficha maneno kuwa: "Ni marufuku kwa mtu yeyote au shirika lolote au kundi lolote la watu isipokuwa Serikali kuunda au kuweka nchini jeshi la aina yeyote."

Na Ibara ya 147(2) inaongeza kwa kusema: "Serikali ya Jamhuri ya Muungano inaweza, kwa mujibu wa sheria, kuunda na kuweka nchini majeshi ya aina mbalimbali kwa ajili ya ulinzi na usalama wa ardhi na watu wa Tanzania."

Na Ibara ya 148 inamalizia mnyororo wote wa mamlaka kwa kusema: "Rais ndiye Amiri Jeshi Mkuu wa majeshi yote ya Jamhuri ya Muungano."

Hapo ndipo siri ya kauli ya Chacha inapobainika. Nani ni Rais? Rais ni Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi kwa mujibu wa Katiba ya CCM Ibara ya 119 inayosema Mwenyekiti ndiye kiongozi mkuu wa chama na ndiye anayeteuliwa kugombea Urais. Hivyo mnyororo wa kikatiba na kisiasa ni huu: CCM inamzalisha Mwenyekiti, Mwenyekiti anakuwa mgombea Urais, akishinda anakuwa Rais, Rais anakuwa Amiri Jeshi Mkuu, na Amiri Jeshi Mkuu ndiye mmiliki na kiongozi mkuu wa JWTZ, Polisi na Usalama wa Taifa. Hivyo kwa sayansi ya siasa, CCM ndio mmiliki wa vyombo vya dola.

Wachambuzi mbalimbali wa Katiba na siasa wamezungumza na kukubaliana na Chacha.

Dkt Peter Nathan, Mwanasheria wa Katiba, anasema:

" Kisheria, neno Serikali maana yake ni Executive inayoongozwa na Rais. Na Rais kwa mujibu wa mfumo wetu wa vyama vingi lazima atoke kwenye chama. Chama kilichopo madarakani ni CCM. Hivyo kwa tafsiri ya kikatiba, anayemiliki Serikali ndiye anayemiliki vyombo vya dola. Katiba ya CCM Ibara ya 119 inasema Mwenyekiti ndiye kiongozi mkuu. Hivyo mnyororo wa kisheria ni CCM - Serikali - Jeshi. Chacha amesema ukweli wa kisheria ambao mawakili wengi wanaogopa kuusema kwa sababu ya siasa."

Dkt. Asha Suleiman, Mchambuzi wa Itikadi za Vyama kutoka Zanzibar, anasema:

"Hakuna nchi duniani ambapo jeshi ni la wananchi moja kwa moja bila kupitia chama. Hata Marekani jeshi ni la Amiri Jeshi Mkuu ambaye ni Rais wa chama kilichoshinda. Uingereza jeshi ni la The Crown lakini Crown inaongozwa na chama kilichoshinda Ubunge. China ni Jeshi la Communist Party. Hivyo nadharia ya Chacha ya kusema vyombo vya dola ni mali ya CCM ndio uhalisia wa sayansi ya siasa duniani kote. Hata upinzani ukichukua nchi kesho, jambo la kwanza watafanya ni kumiliki JWTZ, Polisi na Usalama."

Mwalimu Thomas Ngubila, Mchambuzi wa Historia ya TANU na CCM, anasema:

" JWTZ ni mtoto wa kuzaa wa CCM. Polisi ilianzishwa na Waingereza lakini ilitaifishwa na TANU mwaka 1961. Usalama wa Taifa ni chombo cha chama tawala kuanzia mwaka 1963. Hivyo Chacha yupo sahihi kihistoria na kikatiba. Bila CCM hakuna JWTZ. Na bila CCM hakuna Serikali."

Bi. Zainab Hussein, Mchambuzi wa Siasa za Uchaguzi Afrika, anasema:

"Hoja ya pili ya Chacha ya kusomba watu kwa mabasi na kuwalipa posho ndio sayansi ya kampeni duniani kote. Marekani wanaita busing na voter mobilization, Kenya wanaita mobilization, Uingereza wanaita canvassing. Tanzania CCM inaita oganaizesheni. Hakuna chama duniani kinachojaza uwanja wa mikutano kwa watu wa miguu. Lazima ulipe na kusafirisha. Chacha yupo sahihi na hata upinzani wanafanya hivyo lakini wanajifanya hawafanyi kwa unafiki."

Bwana Felix Kibwana, Mchambuzi wa masuala ya siasa, anasema:

"Katiba ya CCM inasema Chama ndicho kinachoongoza dola na jamii. Dola bila jeshi hakuna. Hivyo CCM lazima imiliki jeshi kulinda Mapinduzi ya 1964 na Muungano. Ibara ya 147(3) ya Katiba ya Jamhuri inasema askari haruhusiwi kujiunga na chama cha siasa lakini haisemi chama hakiwezi kumiliki askari. Tofauti iko hapo. Chama kinamiliki jeshi kama taasisi, sio askari mmoja mmoja. Ni kama kampuni inamiliki gari, sio dereva."

Dkt. Donald Mzava, Mchambuzi wa Mahusiano ya Kimataifa, anahitimisha:

"Nadharia ya State-Party Fusion ndio inayofanya kazi Tanzania. Serikali na Chama ni kitu kimoja. Wananchi wanapiga kura lakini kura zinasimamiwa na chama tawala na vyombo vyake. Ndio maana Chacha anasema viongozi wote wamewekwa na CCM na sio na wananchi. Ni ukweli mtupu. Hata Marekani Joe Biden na Donald Trump wanaweka majaji, mawaziri na majenerali wao. Hakuna tofauti. Hata upinzani ukichukua nchi utaweka watu wake na kumiliki jeshi kulinda utawala wake. Ndio kanuni ya madaraka."

Comments

#maratotv

RAIS RUTTO AAMBATANA NA ODINGA NCHINI CHINA

Rais wa Jamhuri ya Kenya Mh William Rutto na mke wake wamewasili nchini China kuhudhuria mkutano wa wakuu wa nchi na Serikali wa Jukwaa la ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC). Katika ziara hiyo ameambatana na waziri mkuu mstaafu wa nchi hiyo Raila Odinga ambaye pia anapigiwa kampeni ili aweze kushinda nafasi ya Uenyekiti wa AU.

WIZARA YA MALI ASILI YASISITIZA MATUMIZI YA SHERIA NA KANUNI KATIKA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA UHIFADHI

Na.Joyce Ndunguru, Morogoro. Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii anaeshughulikia Maliasili, Kamishna wa Polisi Benedict Wakulyamba asisitiza matumizi ya sheria na kanuni katika utekelezaji wa shughuli mbalimbali za uhifadhi. Kamishna Wakulyamba ameyasema hayo leo Septemba 1, 2024 wakati wa ziara ya kikazi aliyoifanya katika ofisi za Makao Makuu ya TAWA yaliyopo Mkoani Morogoro kwa lengo la kuongea na watumishi ili kuimarisha utendaji kazi pamoja na kukagua maeneo ya kazi. "Kama wahifadhi tunapaswa kufahamu sheria zote zinazosimamia masuala ya uhifadhi zilizopo katika Taasisi zetu pamoja na za Taasisi zingine za uhifadhi zilizopo ndani ya Wizara ya Maliasili na utalii" amesema Kamishna Wakulyamba. "Pamoja na kufahamu sheria na kanuni zilizopo ndani ya Wizara yetu, ni vyema kufahamu na kuzingatia sheria nyingine za Nchi ambazo zinatuzunguka ili ziweze kutusaidia katika utekelezaji wa majukumu yetu mfano sheria inayohusiana na ukusanyaji wa vielelezo kuanzia kw...

Rais Dkt. Samia Awasili China Kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jukwaa la Ushirikiano Kati ya China na Africa FOCAC

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Beijing Capital nchini China kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Wakuu wa nchi na Serikali wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) tarehe 03 Septemba, 2024.

MAKOMANDOO MIAKA 60 YA JWTZ,HAIJAWAHI KUTOKEA

Makomandoo ya jeshi la ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ)wamekuwa kivutio cha aina yake kwenye kikele cha maadhimisho ya miaka 60 ya tangu kuanzishwa kwa jeshi hilo. Katika sherehe hizo ambazo zimefanyika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ameshiriki kwenye kilele cha Maadhimisho ya Miaka 60 ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania katika uwanja huo wa Uhuru Jijini Dar es Salaam, leo tarehe 1 Septemba, 2024. Rais ameonesha kujivunia na kulipongeza JWTZ kwa kufanya kazi kwa kufuata misingi ya kuanzishwa kwake huku akitumia nafasi hiyo kuwapongeza Marais waliomtangulia kwa kazi kubwa waliyofanya wakati wa uongozi wao kwa kuliongoza vema jeshi hilo.

Meli ya Mv. Serengeti yapinduka na kuzama katika Bandari ya Mwanza kusini

 Meli Mv.Serengeti imepinduka na kuzama kwenye bandari ya mwanza kusini.  Meli hiyo imepinduka na kuzama disemba 26 majira ya saa Saba za usiku.  Tukio hilo limetokea meli hiyo ikiwa imefungwa katika gati la bandari ya mwanza kusini.  Kampuni ya meli Tanzania(Tashico) imethibitisha meli ya Mv. Serengeti kupinduka na kuzama upande mmoja wa nyuma.  Kwa Mujibu wa Taarifa iliyotolewa na kitengo cha Masoko na Uhusiano kwa Umma cha Kampuni hiyo inaeleza kuwa Tashico imeshirikiana na Timu mbalimbali za Wataalam kutoka Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania(TASAC), Mamlaka ya Usimamizi wa bandari (TPA) na wadau wengine katika Juhudi za Uokoaji.  Kwa Mujibu wa Taarifa hiyo,Taarifa rasmi ya chanzo cha Tatizo itatolewa Meli hiyo itakapokuwa imeinuliwa na Uchunguzi wa kubaini Tatizo utakapokuwa umefanyika. Meli ya Mv.Serengeti inadaiwa kusitisha safari zake kwenye ziwa Victoria mwaka 2016  Meli ya Mv.Serengeti imepinduka na kuzama katika...

Jenerali Jacob Mkunda Atembelea Meli Tiba ya China Aridhishwa na Huduma

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Jacob John Mkunda ametembelea meli tiba ya Jeshi la Ukombozi la Watu wa China Peace Ark ili kuona matibabu yanavyofanyika. Jenerali Mkunda amefurahishwa na namna wataalam wa tiba wa Jeshi la China walivyotoa matibabu kwa kushirikiana na wataalam wa tiba wa JWTZ . Meli tiba ya jeshi la China imekuja hapa nchini na kutia nanga kwenye bandari ya Dar Es Salaam kutoa matibabu mbalimbali kwa wananchi ikiwa ni muendelezo wa maadhimisho ya miaka 60 tangu kuanzishwa kwa JWTZ  na ushirikiano wa miaka 60 baina ya JWTZ na Jeshi la Ukombozi la Watu wa  China. Matibabu hayo yalianza kutolewa tarehe 18 Julai 2024 hadi tarehe 22 Julai 2024. Meli tiba hiyo itaondoka hapa nchini tarehe 23 Julai mwaka huu.

AMIRI JESHI MKUU AKAGUA GWARIDE LA MIAKA 60 YA JWTZ

 Mapema leo asubuhi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Mhe.Dkt,Samia Suluhu Hassan akikagua Gwaride Maalumu la Maadhimisho ya Miaka 60 ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Uwanja wa Uhuru leo September 01,2024. Rais Samia Suluhu Hassan amesisitiza kuwa jeshi la ulinzi la Wananchi Tanzania si jeshi la Uvamizi bali ni jeshi la ulinzi wa Wananchi Tanzania Amewahakikishia wanajeshi kufanya kazi kifua mbele,kuwa amiri jeshi mkuu yuko pamoja nao wakati wote.

Mbunge wa Bukoba Vijijini ameaga Sifa Kedekede Kwa Rais Samia

 Na Angela Sebastian; Bukoba  MBUNGE wa jimbo la Bukoba vijijini Dk. Jasson Rweikiza amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Samia Suluhu Hassan kwa niaba ya wananchi wa jimbo hilo, kwa kuwapatia zaidi ya shilingi bilioni 19 kwa ajili ya ujenzi wa madaraja mawili ambayo ni lango la kutoka na kuingia ndani ya mkoa wa Kagera. Ametoa shukrani hizo wakati akiongea wananchi mbalimbali waliofika katika viwanja vya Rweikiza pre and Primary school iliyoko eneo la Kyetema Bukoba vijijini, kwa kwa ajili ya kumbukizi ya miaka 100 ya kuzaliwa baba wa mbunge huyo aliyekuwa akiitwa Samsoni Rweikiza.  Rweikiza amebainisha kuwa,Dk. Samia Suluhu Hassan ni Rais mwenye upendo amekubali kutoa mabilioni ya fedha kwa ajili ya Bukoba Vijijini na ndiyo maana tunasema atakuwa kiongozi wetu kwa awamu nyingine tena,tunapaswa kila mmoja kumuunga mkono. ametaja madaraja hayo kuwa ni Karebe ambalo limetengewa kiasi cha shilingi bil.9.3 kwa ajili ya ukarabati mkubwa kutokana na daraja ...

Jenerali ameacha alama ya uzalendo na kujitoa kwa ajili ya Taifa

*📌 Serikali itaenzi na kuthamini mchango wake* *📌 Asema Jenerali Musuguri alijitolea kuhakikisha Tanzania inabaki na amani na usalama* *📌 Asema alikuwa mstari wa mbele kuliokoa Taifa* *📌 Aiasa jamii kuacha alama katika maisha ya kila siku* *📌 Dkt. Biteko aongoza mamia ya watu mazishi ya Jenerali Musuguri Butiama* Na Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amesema kuwa  aliyewahi kuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Mstaafu David Bugozi Musuguri alijitolea  kuhakikisha Tanzania inabaki kuwa na amani, usalama na mshikamano pamoja na kuifundisha jamii  moyo wa dhati wa kuilinda nchi. Dkt. Biteko amesema hayo leo Novemba 4, 2024 Butiama mkoani Mara wakati akiwasilisha salamu za Serikali kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika mazishi ya Jenerali Mstaafu Musuguri. “ Katika  uhai wa kila mmoja wetu ni jambo gani mtu atakumbukwa nalo, baba huyu a...

Majaliwa Achangisha Shilingi Milioni 900 za Ujenzi wa Kanisa Kuu Lindi

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameendesha harambee na kuchangisha sh. milioni 928.67  za ujenzi wa kanisa kuu tarajiwa la Mt. Andrea Kagwa la Jimbo Katoliki la Lindi. Kati ya fedha hizo, sh. milioni 464.3 ni fedha taslimu na nyingine kati ya hizo zimeshawekwa benki na sh. milioni 464.37 bado ni ahadi. Awamu ya kwanza ya ujenzi huo, inatarajiwa kugharimu sh. milioni 700. Akizungumza na waumini na wadau mbalimbali waliohudhuria harambee iliyofanyika Ruangwa mjini, leo mchana (Jumamosi, Julai 27, 2024), Waziri Mkuu amewataka waliotoa ahadi wazikamilishe mapema ili kazi ya ujenzi isikwame. "Ninawashukuru sana wote mliofika na wote waliochangia ujenzi wa kanisa tarajiwa. Ninawaomba walioahidi, wakamilishe ahadi zao mapema ili kazi ianze kwani ramani ipo, mafundi wapo tayari,  wasimamizi wa ujenzi wapo," amesisitiza.  Waziri Mkuu amesema uamuzi wa Baba Askofu wa Jimbo Katoliki la Lindi, Mhashamu Askofu Wolfgang Pisa kuanza ujenzi wa kanisa kuu la jimbo hilo, ni utekelezaji ...