Na Mwanamkuu Mwandoro, Tanga.
KAMISHNA wa ardhi msaidizi mkoa wa Tanga Jabir Singano amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi katika uzinduzi wa kliniki ya ardhi unaotarajiwa kuanza kufanyika kesho katika Wilaya ya Muheza katika viwanja vya stendi ya bombani ambapo pamoja na huduma nyingine migogoro ya ardhi itafanyiwa kazi sambamba na utoaji wa hati Kwa wale waliokamilisha hatua zote.
Kliniki hiyo ambayo hufanyika Kila mwaka katika mikoa yote nchini ikiwa na lengo la kutoa elimu Kwa jamii juu ya ardhi pamoja na kusogeza karibu huduma zinazotolewa chini ya wizara ya Ardhi
Akizungumza na waandshi wa habari kuelekea ufunguzi huo wa kliniki ya ardhi utakao dumu kwa takribani siku kumi kuanzia tarehe 22/9/2026 - 3/10/2026 amesema kuwa migogoro ya ardhi mkoa wa Tanga imepungua kutokana na elimu iliyokuwa ikiendelea kutolewa Kwa jamii.
Amewataka wananchi kuacha kutumia madalali wakati wanapohitaji umiliki wa ardhi ambao wengi wamekuwa wakiwaingiza katika migogoro mbalimbali badala yake kuzitumia ofisi za ardhi pamoja na Halmashauri husika.
Aidha amewataka wamiliki wa ardhi mkoani humo ikiwemo wawekezaji kuzingatia mikataba waliyopewa baada ya kumilikishwa ardhi ikiwa ni pamoja na kuendeleza maeneo yao sambamba na kuweka alama za mipaka ili kuondokana na migogoro ya ardhi baina yao na wananchi ambayo inaweza kujitokeza.
Kwa Upande wake msajili wa hati msaidizi mkoa wa Tanga Mwajuma Kihiyo amewataka wananchi kutovamia maeneo wanayoyakuta wazi kwani maeneo mengine huachwa wazi Kwa sababu maalimu ikiwemo kuruhusu maji kupita au huwa ni sehemu za mabondeni.
Aidha Kihiyo pia aliongeza kuwa lengo kuu la kliniki hiyo likiwa ni kusogeza huduma karibu zaidi na wananchi sambamba na kutatua changamoto za ardhi zinazowakabili



Comments
Post a Comment