Na Wellu Mtaki, Geita
Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini (GST) imeendelea kutoa elimu kwa wananchi na wadau wa sekta ya madini kuhusu huduma za uchunguzi wa sampuli za miamba, mawe, udongo na maji, hatua inayolenga kuwawezesha kupata taarifa sahihi za kisayansi kwa ajili ya utafiti na shughuli za uzalishaji wa madini.
Akizungumza wakati wa Maonesho ya Kimataifa ya Teknolojia ya Madini yanayoendelea mkoani Geita, Fundi Sanifu Mkuu kutoka GST, Gideon Nshange, alisema taasisi hiyo ina uwezo wa kufanya uchunguzi wa aina mbalimbali za sampuli za madini na kimazingira.
Nshange alisema maabara ya GST hufanya uchunguzi wa madini mbalimbali, ikiwemo dhahabu, shaba, fedha na madini mengine ya msingi, sambamba na uchunguzi wa miamba, udongo na sampuli za maji zinazohusiana na mazingira.
“Tunafanya sampuli za miamba, mawe na udongo, lakini pia tunafanya sampuli za maji kwa maana ya sampuli za kimazingira. Pia tunafanya tafiti za vitu mbalimbali, ikiwemo utafiti unaohusiana na dhahabu,” alisema.
Alisema ushiriki wa GST katika maonyesho hayo unalenga kuwafahamisha wananchi na wadau wa sekta ya madini kuhusu huduma zinazotolewa na taasisi hiyo, huku akiwahimiza kutumia wataalamu na maabara za GST kupata taarifa sahihi kuhusu maeneo yao.
Kwa mujibu wa Nshange, taarifa zinazopatikana kupitia uchunguzi wa kitaalamu zinaweza kuwasaidia wananchi na wachimbaji kufanya maamuzi yenye msingi wa taarifa za kisayansi katika shughuli za utafiti, uchimbaji na uzalishaji wa madini.
Aidha, alisema maonyesho hayo yamepokelewa kwa mwitikio mkubwa na wananchi wa Geita, hususan wachimbaji wa dhahabu, ambao wamekuwa wakifika katika banda la GST kupata elimu na taarifa kuhusu huduma za uchunguzi wa sampuli katika maeneo wanayofanyia shughuli za uchimbaji.
“Wengi wa wananchi walioko katika mkoa huu ni wachimbaji wa dhahabu, kwa hiyo wamekuwa wakihudhuria katika banda letu kwa ajili ya kupata taarifa za uchunguzi katika maeneo yao wanayofanyia uchimbaji wa madini ya dhahabu,” alisema.
Aliongeza kuwa mwitikio huo unaonyesha umuhimu wa wananchi na wadau wa sekta ya madini kupata elimu na taarifa sahihi za kisayansi kabla na wakati wa kufanya shughuli za utafiti na uchimbaji wa ma


Comments
Post a Comment