Tpa Yawakutanisha Wadau wa Bandari Kavu

GEORGE MARATO TV
0


 NA MWANDISHI WETU,DAR ES SALAAM

MENEJIMENTI ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) imewakutanisha Wadau wa Bandari Kavu katika kikao kilicholenga kujadili changamoto,kupokea mawazo na kubadilisha panapohitajika ili kuongeza ufanisi katika uhudumiaji wa shehena.

Kikao hicho kilichofanyika Alhamisi Aprili 16, 2026 Makao Makuu ya TPA kiliongozwa na Mkurugenzi wa Masoko na Uhusiano Dk.George Fasha ambaye katika hotuba yake ya ufunguzi alisema TPA inatambua umuhimu wa Bandari Kavu katika ufanisi wa shughuli za kibandari nchini.

Aidha Dk. Fasha aliwataka washiriki wa kikao hicho kujadili kwa uwazi kuhusu maeneo yanayohitaji maboresho na ufanisi katika kuhamisha,kuhifadhi na kushughulikia shehena ndani na nje ya eneo la Bandari Kuu.

Akizungumza kikaoni hapo,Mwenyekiti wa Chama cha Waendesha Bandari Kavu Nchini (CIDAT)Melickzed Kishange alisema vikao aina hii vina umuhimu mkubwa kwa wadau Bandari Kavu kwani ndio jukwaa litakalojadili na kutatua changamoto zitokanazo na shughuli za uhamishaji wa shehena kutoka bandarini.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top