Dodoma
wa Viti Maalum Mkoa WA Mara Agnes Marwa amechaguliwa kuwa Mjumbe wa Kamati ya Bunge Sports Club ukifuata mbunge leo katika ukumbi wa Msekwa Bungeni jijini Dodoma.
Katika uchaguzi huo ulioshirikisha Waheshimiwa Wabunge zaidi ya Kumi na Tano, Agnes Marwa aliibuka mshindi baada ya kupata kura za kutosha zilizompa ushindi wa kuingia katika Kamati Tendaji ya klabu hiyo yenye wajumbe watano.
Kamati hii kazi yake ni pamoja na kuratibu shughuli za michezo kwa wabunge.
Sauti mara baada ya kutangazwa kwa matokeo, Marwa aliwashukuru wabunge kwa imani waliyoonesha kwake na kuahidi kutekeleza majukumu yake kwa uadilifu, uwajibikaji na uwajibikaji. Alisema michezo ni nyenzo muhimu ya kuimarisha afya, mshikamano na mahusiano mema miongoni mwa wabunge, hivyo atahakikisha Bunge Sports Club inazidi kuwa imara na yenye mafanikio.
Kwa ushindi huo, Agnes Marwa anaungana na wengine wa Kamati Tendaji watakaosimamia mipango na maendeleo ya Bunge Sports Club kwa kipindi cha Miaka Mitano.

