Skip to main content

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Waziri Mavunde Azindua Rasmi Shughuli Za Uchimbaji Madini Porcupine North- Chunya Mbeya


▪️Ni Leseni Hodhi zilizorudi Serikalini baada ya kumalizika kesi na wawekezaji

▪️Mapato ya Serikali kuongezeka kupitia mrabaha na kodi mbalimbali

▪️ Waziri Mavunde asisitiza kuongeza utafiti zaidi ili kuongeza uzalishaji wa dhahabu

▪️Wachimbaji wadogo nao wapatiwa Leseni kuongeza uzalishaji


📍 *Chunya- Mbeya*

Waziri wa Madini Mhe. Anthony Mavunde amezindua rasmi shughuli za uchimbaji madini katika mgodi wa Porcupine North- uliopo Makongorosi Wilayani Chunya Mkoa wa Mbeya unaomilikiwa na Kampuni ya Shanta Gold Mining Limited na kusema kuwa hatua hiyo ni matunda ya uamuzi wa Serikali kurudisha leseni ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuhakikisha unawekwa utaratibu mzuri wa kuongeza mapato ya nchi kupitia sekta ya madini.

Waziri Mavunde ameyasema hayo leo Aprili 03, 2025 katika hafla ya Uzinduzi wa Shughuli za Uchimbaji Madini Porcupine North – Kata ya Mkola, Makongorosi Wilayani Chunya Mkoa wa Mbeya.

“Eneo hili ni eneo ambalo Leseni hodhi zimerudi serikalini kwa mujibu wa sheria. Baada ya kumalizika shauri la kimahakama na mwekezaji wa awali,serikali iliweka utaratibu wa wazi kumpata mwekezaji atakayeendesha eneo hili la uchimbaji na Kampuni ya Shanta Gold Mining Limited ilishinda kwa masharti ya kuanza uchimbaji ndani ya miezi 18,ambapo mashapo yaliyothibitishwa kwa sasa yanafikia wakia 110,000 na upo uwezekano baada ya utafiti zaidi kufikisha mashapo ya wakia 400,000 ambazo kupitia mrabaha,kodi na tozo mbalimbali zitasaidia kuongeza makusanyo ya Serikali” amesema Mavunde 

Aidha, Waziri Mavunde amesema kuwa, Leseni moja iliyokuwa katika eneo la Saza, Mkoa wa Songwe, imekabidhi kwa wachimbaji wadogo ili kuhakikisha kundi hilo linanufaika na rasilimali za madini na kwamba eneo hilo la Saza lililokabidhiwa kwa Wachimbaji Wadogo, linakadiriwa kuwa na mashapo ya dhahabu yenye wakia laki mbili, thamani yake ikiwa ni takriban shilingi trilioni 1.2 kwa bei ya sasa ya dhahabu. 

“Mgodi  huu pia utatoa fursa za ajira kwa Watanzania, kuchangia maendeleo ya jamii kupitia mpango wa Uwajibikaji kwa Jamii (CSR) na kuhakikisha kunakuwepo na ushirikishwaji wa wazawa kupitia sera ya Local Content” Ameongeza Mavunde

Kwa upande wake, Katibu Mkuu Wizara ya Madini Mhandisi Yahya Samamba amesema kuwa tukio la uzinduzi wa shughuli za uchimbaji katika mgodi huo ni ushuhuda wa mazingira mazuri ya uwekezaji hapa nchini Tanzania chini ya uongozi na maelekezo ya Rais Dkt.  Samia Suluhu Hassan na Wasaidizi wake na kwa mgodi huo utakuwa mfano wa kipekee hapa nchini.

Wakizungumza kwa Nyakati tofauti, Mkuu wa Wilaya Chunya Alhaji Mbaraka Alhaji Mbaraka Batenga, kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa Mbeya na Mkuu wa Wilaya ya Songwe Solomon Itunda, kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa Songwe wameleeza wamewapongeza wananchi wa Kata ya Mkola kwa kuruhusu hatua hiyo kufikiwa, kwa kutoa ushirikiano kwa manufaa ya vizazi vilivyopo na vijavyo vya kata hiyo na taifa kwa ujumla.

“Tunakupongeza wewe binafsi Mhe. Waziri Mavunde kwa kufuta leseni zilizokuwa hazifanyiwi kazi, ambazo baada ya kurudisha Serikalini mnaendelea kuwapanga vyema wachimbaji wadogo.” Amesisitiza Alhaj Batenga.

Nao, Mkurugenzi Mwendeshaji wa Kampuni ya Shanta Gold Mining Mhandisi Honest Mrema na Meneja wa Mgodi wa New Luika Gold Mine unaomilikiwa na Kampuni hiyo Mhandisi Exeuper Lyimo wametoa shukrani zao za dhati kwa Serikali kwa upatikanaji wa leseni hizo na hatimaye kuanza uchimbaji na uzalishaji. 

“Kupitia Mgodi huu, Kampuni imeongeza uhai wa maisha ya Migodi yake hapa nchini kutoka mwaka 2031 hadi 2034 na kupitia utafiti tunaoendelea kufanya uhai wa migodi utaongezeka zaidi. Lakini pia, shughuli za uchimbaji madini katika mgodi huu zitafanywa na Kampuni za kitanzania kwa asilimia 100. 

Mgodi wa New Luika imeajiri wafanyakazi 1140 ambapo asilimia 40 ni wakazi wanaozunguka eneo la mradi na kuanza kwa mgodi huu kutasaidia kuongeza wafanyakazi zaidi ya 100 ambapo asilimia 60 yao ni vijana kutoka katika maeneo haya ya Porcupine.” Ameongeza Mhandisi Mrema.





Comments

#maratotv

RAIS RUTTO AAMBATANA NA ODINGA NCHINI CHINA

Rais wa Jamhuri ya Kenya Mh William Rutto na mke wake wamewasili nchini China kuhudhuria mkutano wa wakuu wa nchi na Serikali wa Jukwaa la ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC). Katika ziara hiyo ameambatana na waziri mkuu mstaafu wa nchi hiyo Raila Odinga ambaye pia anapigiwa kampeni ili aweze kushinda nafasi ya Uenyekiti wa AU.

WIZARA YA MALI ASILI YASISITIZA MATUMIZI YA SHERIA NA KANUNI KATIKA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA UHIFADHI

Na.Joyce Ndunguru, Morogoro. Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii anaeshughulikia Maliasili, Kamishna wa Polisi Benedict Wakulyamba asisitiza matumizi ya sheria na kanuni katika utekelezaji wa shughuli mbalimbali za uhifadhi. Kamishna Wakulyamba ameyasema hayo leo Septemba 1, 2024 wakati wa ziara ya kikazi aliyoifanya katika ofisi za Makao Makuu ya TAWA yaliyopo Mkoani Morogoro kwa lengo la kuongea na watumishi ili kuimarisha utendaji kazi pamoja na kukagua maeneo ya kazi. "Kama wahifadhi tunapaswa kufahamu sheria zote zinazosimamia masuala ya uhifadhi zilizopo katika Taasisi zetu pamoja na za Taasisi zingine za uhifadhi zilizopo ndani ya Wizara ya Maliasili na utalii" amesema Kamishna Wakulyamba. "Pamoja na kufahamu sheria na kanuni zilizopo ndani ya Wizara yetu, ni vyema kufahamu na kuzingatia sheria nyingine za Nchi ambazo zinatuzunguka ili ziweze kutusaidia katika utekelezaji wa majukumu yetu mfano sheria inayohusiana na ukusanyaji wa vielelezo kuanzia kw...

Rais Dkt. Samia Awasili China Kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jukwaa la Ushirikiano Kati ya China na Africa FOCAC

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Beijing Capital nchini China kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Wakuu wa nchi na Serikali wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) tarehe 03 Septemba, 2024.

Wananchi Serengeti Wamtaja Dkt Rhimo Nyansaho Kama Chachu ya Maendeleo Kwao

Na Shomari Binda-GMTV  WANANCHI Wilaya ya Serengeti mkoani Mara wamemtaja Dkt.Rhimo Nyansaho kama chachu ya maendeleo kupitia taasisi yake ya Nyansaho Foundation. Wakizungumza kwa nyakati tofauti na GMTV wananchi hao wamesema kwa kipindi kirefu mchango wake umeonekana katika kuisaidia jamii. Wamesema ukifika Jimbo la Serengeti kila Kata na Kijiji huwezi kukosa mkono wa Dkt.Nyansaho kuchangia na kusaidia jamii kuanzia elimu,afya,maji na masuala mengine ya jamii. Mmoja wa wananchi hao aliyejitambulisha kwa jina la Mwita Sagati amesema wapo watu wanaojitokeza kusaidia jamii kipindi cha uchaguzi kwa kulenga kupata uongozi lakini imekuwa tofauti kwa Dkt.Nyansaho. Sagati amesema iwapo atajitokeza kuomba nafasi ya ubunge wapo tayari kumpambania na kumchagua ili aweze kuendelea kutoa mchango wake katika kusaidia jamii. " Tunashukuru sana mchango wa Dkt.Nyansaho kwa kuchangia shughuli za maendeleo hapa Serengeti. " Wengine huwa wanakuja nyakati za uchaguzi lakini huyu mchango wake ni ...

MAKOMANDOO MIAKA 60 YA JWTZ,HAIJAWAHI KUTOKEA

Makomandoo ya jeshi la ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ)wamekuwa kivutio cha aina yake kwenye kikele cha maadhimisho ya miaka 60 ya tangu kuanzishwa kwa jeshi hilo. Katika sherehe hizo ambazo zimefanyika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ameshiriki kwenye kilele cha Maadhimisho ya Miaka 60 ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania katika uwanja huo wa Uhuru Jijini Dar es Salaam, leo tarehe 1 Septemba, 2024. Rais ameonesha kujivunia na kulipongeza JWTZ kwa kufanya kazi kwa kufuata misingi ya kuanzishwa kwake huku akitumia nafasi hiyo kuwapongeza Marais waliomtangulia kwa kazi kubwa waliyofanya wakati wa uongozi wao kwa kuliongoza vema jeshi hilo.

Meli ya Mv. Serengeti yapinduka na kuzama katika Bandari ya Mwanza kusini

 Meli Mv.Serengeti imepinduka na kuzama kwenye bandari ya mwanza kusini.  Meli hiyo imepinduka na kuzama disemba 26 majira ya saa Saba za usiku.  Tukio hilo limetokea meli hiyo ikiwa imefungwa katika gati la bandari ya mwanza kusini.  Kampuni ya meli Tanzania(Tashico) imethibitisha meli ya Mv. Serengeti kupinduka na kuzama upande mmoja wa nyuma.  Kwa Mujibu wa Taarifa iliyotolewa na kitengo cha Masoko na Uhusiano kwa Umma cha Kampuni hiyo inaeleza kuwa Tashico imeshirikiana na Timu mbalimbali za Wataalam kutoka Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania(TASAC), Mamlaka ya Usimamizi wa bandari (TPA) na wadau wengine katika Juhudi za Uokoaji.  Kwa Mujibu wa Taarifa hiyo,Taarifa rasmi ya chanzo cha Tatizo itatolewa Meli hiyo itakapokuwa imeinuliwa na Uchunguzi wa kubaini Tatizo utakapokuwa umefanyika. Meli ya Mv.Serengeti inadaiwa kusitisha safari zake kwenye ziwa Victoria mwaka 2016  Meli ya Mv.Serengeti imepinduka na kuzama katika...

Mbunge wa Bukoba Vijijini ameaga Sifa Kedekede Kwa Rais Samia

 Na Angela Sebastian; Bukoba  MBUNGE wa jimbo la Bukoba vijijini Dk. Jasson Rweikiza amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Samia Suluhu Hassan kwa niaba ya wananchi wa jimbo hilo, kwa kuwapatia zaidi ya shilingi bilioni 19 kwa ajili ya ujenzi wa madaraja mawili ambayo ni lango la kutoka na kuingia ndani ya mkoa wa Kagera. Ametoa shukrani hizo wakati akiongea wananchi mbalimbali waliofika katika viwanja vya Rweikiza pre and Primary school iliyoko eneo la Kyetema Bukoba vijijini, kwa kwa ajili ya kumbukizi ya miaka 100 ya kuzaliwa baba wa mbunge huyo aliyekuwa akiitwa Samsoni Rweikiza.  Rweikiza amebainisha kuwa,Dk. Samia Suluhu Hassan ni Rais mwenye upendo amekubali kutoa mabilioni ya fedha kwa ajili ya Bukoba Vijijini na ndiyo maana tunasema atakuwa kiongozi wetu kwa awamu nyingine tena,tunapaswa kila mmoja kumuunga mkono. ametaja madaraja hayo kuwa ni Karebe ambalo limetengewa kiasi cha shilingi bil.9.3 kwa ajili ya ukarabati mkubwa kutokana na daraja ...

Jenerali Jacob Mkunda Atembelea Meli Tiba ya China Aridhishwa na Huduma

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Jacob John Mkunda ametembelea meli tiba ya Jeshi la Ukombozi la Watu wa China Peace Ark ili kuona matibabu yanavyofanyika. Jenerali Mkunda amefurahishwa na namna wataalam wa tiba wa Jeshi la China walivyotoa matibabu kwa kushirikiana na wataalam wa tiba wa JWTZ . Meli tiba ya jeshi la China imekuja hapa nchini na kutia nanga kwenye bandari ya Dar Es Salaam kutoa matibabu mbalimbali kwa wananchi ikiwa ni muendelezo wa maadhimisho ya miaka 60 tangu kuanzishwa kwa JWTZ  na ushirikiano wa miaka 60 baina ya JWTZ na Jeshi la Ukombozi la Watu wa  China. Matibabu hayo yalianza kutolewa tarehe 18 Julai 2024 hadi tarehe 22 Julai 2024. Meli tiba hiyo itaondoka hapa nchini tarehe 23 Julai mwaka huu.

AMIRI JESHI MKUU AKAGUA GWARIDE LA MIAKA 60 YA JWTZ

 Mapema leo asubuhi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Mhe.Dkt,Samia Suluhu Hassan akikagua Gwaride Maalumu la Maadhimisho ya Miaka 60 ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Uwanja wa Uhuru leo September 01,2024. Rais Samia Suluhu Hassan amesisitiza kuwa jeshi la ulinzi la Wananchi Tanzania si jeshi la Uvamizi bali ni jeshi la ulinzi wa Wananchi Tanzania Amewahakikishia wanajeshi kufanya kazi kifua mbele,kuwa amiri jeshi mkuu yuko pamoja nao wakati wote.

Jenerali ameacha alama ya uzalendo na kujitoa kwa ajili ya Taifa

*📌 Serikali itaenzi na kuthamini mchango wake* *📌 Asema Jenerali Musuguri alijitolea kuhakikisha Tanzania inabaki na amani na usalama* *📌 Asema alikuwa mstari wa mbele kuliokoa Taifa* *📌 Aiasa jamii kuacha alama katika maisha ya kila siku* *📌 Dkt. Biteko aongoza mamia ya watu mazishi ya Jenerali Musuguri Butiama* Na Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amesema kuwa  aliyewahi kuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Mstaafu David Bugozi Musuguri alijitolea  kuhakikisha Tanzania inabaki kuwa na amani, usalama na mshikamano pamoja na kuifundisha jamii  moyo wa dhati wa kuilinda nchi. Dkt. Biteko amesema hayo leo Novemba 4, 2024 Butiama mkoani Mara wakati akiwasilisha salamu za Serikali kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika mazishi ya Jenerali Mstaafu Musuguri. “ Katika  uhai wa kila mmoja wetu ni jambo gani mtu atakumbukwa nalo, baba huyu a...