Rais mteule Donald Trump amemteua mwenyekiti-mwenza wa timu yake ya kampeni, Susie Wiles, kuwa White House Chief of Staff wa Marekani

GEORGE MARATO TV
0


 Rais mteule Donald Trump amemteua mwenyekiti-mwenza wa timu yake ya kampeni, Susie Wiles, kuwa White House Chief of Staff wa Marekani. Anakua mwanamke wa kwanza kuhudumu katika nafasi hiyo.

Nafasi ya WH Chief of Staff ni moja ya nafasi zenye ushawishi mkubwa katika utawala wa Marekani, ambapo mhusika huyu hutumika kama mshauri mkuu wa rais na kuhakikisha utendaji wa Ikulu unafanyika kwa ufanisi. Haya ni baadhi ya majukumu ya nafasi hii:

1. Ratiba na Mipangilio: Anasimamia ratiba ya kila siku ya rais, akihakikisha kuwa mikutano na majukumu yote yanazingatia malengo ya utawala.

2. Mshauri na Mlinda Mlango: Akiwa mshauri wa karibu zaidi wa rais, anahusika na kuchuja taarifa na watu wanaofika kwa rais ili kuhakikisha muda na nishati ya rais vinatumika vyema.

3. Mkurugenzi ya Sera na Watumishi: Anasimamia washauri wakuu na watumishi wa Ikulu, akihakikisha kuwa wote wanashirikiana katika kufanikisha ajenda na sera za rais.

4. Kujenga Mahusiano Muhimu: Akitumika kama kiunganishi kati ya Ikulu, Bunge, vikundi vya kisiasa, na wadau wengine, WH Chief of Staff anahusika katika mawasiliano na majadiliano kwa niaba ya rais.

5. Ushughulikiaji wa Migogoro: Katika nyakati za migogoro ya kitaifa au kimataifa, WH Chief of Staf husaidia kutoa mwelekeo wa kimkakati na kuhakikisha utulivu katika utendaji wa Ikulu.

Susie Wiles ni miongoni mwa wanamikakati maarufu wa kisiasa nchini Marekani, akijulikana kwa ufanisi wake katika usimamizi wa kampeni za chama cha Republican. Ana uzoefu wa kipekee katika kampeni za kisiasa, na amekuwa mshauri wa karibu wa Donald Trump tangu kampeni yake ya urais ya mwaka 2016. Wiles alikua na nafasi muhimu katika kuhakikisha ushindi wa Trump katika jimbo la Florida, ambalo ni la kimkakati sana, katika uchaguzi wa 2016, 2020 na 2024. Kwa sasa, ni mmoja wa viongozi wa kampeni ya Trump ya 2024 kama mwenyekiti mwenza.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top