Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Mhe. Dkt. Rhimo Nyansaho (Mb), amezindua rasmi mfumo wa kisasa wa kidigitali wa Ngome SACCOS Limited, unaolenga kuboresha na kurahisisha utoaji wa huduma kwa wanachama. Uzinduzi huo umefanyika 19 Novemba, 2026, jijini Dar es Salaam, wakati wa Mkutano Mkuu wa 21 wa chama hicho uliofanyika katika Ukumbi wa Brigade Mess. Akizungumza katika hafla hiyo, Waziri Nyansaho amepongeza uongozi wa Ngome SACCOS kwa kutumia teknolojia katika kuboresha huduma, akisisitiza kuwa Serikali inahimiza taasisi za fedha na vyama vya ushirika kuimarisha mifumo ya kidigitali ili kuongeza uwazi, kupunguza urasimu na kuwapatia wanachama huduma kwa haraka na ufanisi. Mfumo huo unatarajiwa kupunguza matumizi ya karatasi, kuondoa makosa ya kibinadamu na kuimarisha usalama wa kumbukumbu za wanachama. Mwenyekiti wa Bodi ya Ngome SACCOS amesema hatua hiyo ni sehemu ya mkakati wa muda mrefu wa kujenga taasisi imara ya kifedha, yenye uwezo wa kukidhi ongezeko la wa...
Marato tv - Sauti ya Jamii