CHAMWINO
Mbunge wa Jimbo la Chamwino mkoani Dodoma, Mhe. Dkt. Netho Ndilito, amewataka viongozi wa dini katika jimbo hilo kuendelea kutumia nafasi zao kuhamasisha umoja, amani, upendo na mshikamano miongoni mwa wananchi ili kudumisha mahusiano mema katika jamii.
Dkt. Ndilito ameyasema hayo Novemba 19, 2026, alipokutana na kufanya kikao na viongozi wa dini wa Jimbo la Chamwino, ambapo amesisitiza umuhimu wa viongozi hao kuendelea kuwaelimisha waumini na jamii kwa ujumla kuhusu kudumisha amani na mshikamano.
"Twendeni tukasisitize kwa watu wetu kuhakikisha umoja, amani, upendo na mshikamano katika jamii zetu vinaendelea kuimarika," amesema Dkt. Ndilito.
Aidha, amewaomba viongozi hao wa dini kuendelea kuwahamasisha wananchi kushiriki kikamilifu katika shughuli za maendeleo katika maeneo yao, akieleza kuwa maendeleo yanahitaji ushirikiano kati ya Serikali na wananchi.
"Serikali itafanya kwa kipande chake, lakini mwananchi naye ana namna ya kushiriki katika shughuli za maendeleo," amesema Dkt. Ndilito.
Amesisitiza kuwa ushiriki wa wananchi katika shughuli za maendeleo ni muhimu katika kuharakisha upatikanaji wa huduma na kuboresha maisha ya jamii.
Dkt Ndilito alichaguliwa kuwa mbunge wa jimbo la Chamwino hivi karibuni akichukua nafasi ya Mhe. Deogratius Ndejembi, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania










Comments
Post a Comment