Skip to main content

Posts

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Rais Samia Aongoza Watanzania Kuaga Mwili wa Lukuvi

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa katika Matukio tofauti ya picha alipoongoza Watanzania kuaga mwili wa aliyekuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu) na Mbunge wa Jimbo la Isimani, Marehemu Mhe. William Lukuvi katika Viwanja vya Karimjee Jijini Dar es salaam leo Machi 28, 2026. Mhe. Lukuvi alifariki Dunia tarehe 25 Machi 2026 alipokuwa akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Bejamin Mkapa Mkoani Dodoma.

Tume ya Ushindani (Fcc) Yaombwa Kuendeleza Elimu na Kudhibiti Bidhaa Bandia Mkoani Mara

Na Mwandishi wetu Jovina Massano. Baadhi ya wafanyabiashara na wananchi waiomba tume ya ushindani (FCC) kuendelea kuthibiti na kutoa elimu ili kuepuka athari za matumizi ya bidhaa bandia. Hayo yamesemwa na wafanyabiashara wa soko kuu la Manispaa ya Musoma mara baada ya kufikiwa na maafisa wa Tume ya ushindani kupata elimu ya bidhaa bandia,mikataba ya mlaji (mikopo inayotolewa na taasisi za fedha)inayotoa vigezo na masharti vilivyoandaliwa na upande mmoja. Maafisa hao wa ukaguzi bidhaa bandia Mgasi Kalindimya na Thomas Maisory wamewaelimisha wafanyabiashara hao umuhimu wa kutambua  bidhaa wanapofanya manunuzi au kuuza bidhaa zao kwa mtumiaji wa mwisho sambamba na vigezo na masharti  ya mikopo kwa mlaji (mkopaji). Tume ya ushindani (FCC) inaendelea kutoa elimu kwa wafanyabiashara mkoani hapa kuondokana na uuzaji wa bidhaa bandia zinazopelekea kuathiri afya kwa walaji. Akiongea na GMTV Jane Maginga mfanyabiashara wa soko kuu la Musoma  mkazi wa Mwisenge amesema hivi sasa bid...

Wakala wa Vipimo Wadhamiria Kutokomeza Lumbesa

 *Na WMA – DODOMA* Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Vipimo (WMA), Alban Kihulla amewataka watendaji wa Wakala hiyo kuanza ukaguzi wa mazao ya shamba na kupambana zaidi na ufungashaji wa mazao hayo kwa mtindo wa lumbesa. Akifungua Mkutano wa 37 wa Baraza la Wafanyakazi wa WMA, Machi 27, 2026 jijini Dodoma, Kihulla amewasisitiza wajumbe wa Baraza hilo kufikisha ujumbe huo kwa watumishi wote katika maeneo yao kuanza kutekeleza jukumu hilo kikamilifu. “Lakini tunapotekeleza majukumu haya, tuhakikishe haki katika biashara na kulinda mapato ya Serikali,”ametahadharisha. Amesema kuwa katika kipindi cha kuanzia Julai 2025 hadi Machi 2026, WMA imepata mafanikio mbalimbali katika utekelezaji wa majukumu yake ya kumlinda mlaji kupitia uhakiki wa vipimo lakini pia kumekuwepo na changamoto kadhaa. Akidadavua, amesema mafanikio yaliyopatikana yametokana na juhudi, weledi na ushirikiano wa watumishi wote wa Wakala hivyo amewapongeza kwa kazi nzuri wanayoendelea kufanya. “Pamoja na mafanikio hayo,...

Prof. Shemdoe Awaasa Walimu 150 Kuzingatia Mafunzo Nchini India ili Kuwa Mahiri na Kuleta Mageuzi ya Elimu Nchini

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu - TAMISEMI Mhe. Prof. Riziki Shemdoe amewataka walimu 150 wa Amali za Kihandisi wanaokwenda India kuongeza umahiri kuhakikisha wanajifunza kwa bidii ili watakaporejea wawajengee uwezo walimu wengine, na hatimaye kutoa mchango utaokuwa na tija katika kuharakisha mageuzi ya elimu nchini. Prof. Shemdoe ametoa wito huo Machi 26, 2026 kwa walimu hao waliopata fursa ya kwenda nchini India kuongeza umahiri, wakati wa hafla ya kuwaaga walimu hao iliyofanyika Jiji Dar es Salaam. “Nendeni mkajifunze kwa bidii na nidhamu, mkazingatie maadili, jifunzeni mbinu mpya na muwe tayari kuzitumia mtakaporejea, hivyo tunatarajia mtakaporejea mtakuwa nguzo ya kuboresha elimu ya amali katika shule zenu na chanzo cha maarifa kwa walimu wengine,” amesisitiza Prof. Shemdoe. Kwa upande wake, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda amesisitiza kuwa mpango wa mafunzo hayo ni utekelezaji wa sera ya elimu ya lazima ya miaka 10, unaolenga kujenga umahiri wa ufund...

Vijana 521 Waondoka Kwa Ajira Nje ya Nchi, 45 Waenda Ulaya

Na OWM-KAM, Dar es Salaam Serikali imeendelea kufungua na kuimarisha njia salama za uhamiaji wa nguvu kazi kwa kushirikiana na nchi rafiki pamoja na taasisi za kikanda na kimataifa, ikiwa ni juhudi za kuhakikisha Watanzania wanapata ajira zenye staha, kulindwa haki zao na kushiriki kikamilifu katika uchumi wa dunia. Akizungumza katika hafla ya kuwaaga vijana 521 waliopata fursa za ajira nje ya nchi, iliyofanyika Machi 27, 2026 jijini Dar es Salaam, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu -Kazi, Ajira na Mahusiano, Mheshimiwa Deus Sangu, alisema hatua hiyo ni utekelezaji wa maono ya Rais Samia Suluhu Hassan katika kukuza ajira kwa vijana. Alisema Serikali imejipanga kuhakikisha usalama wa Watanzania wanaokwenda kufanya kazi nje ya nchi unalindwa kikamilifu, na kuwahakikishia vijana hao kuwa waende kwa utulivu na kujiamini kwa kuwa Serikali ipo pamoja nao. Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Kitengo cha Ajira, Bi. Jane Sologo, aliwashukuru mawakala binafsi kwa mchango wao mkubwa katika kuwaungan...

Makamu wa Rais Afanya Mazungumzo na Mfalme Mswati III

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, akifanya mazungumzo na Mfalme wa Eswatini, Mswati III kando ya Mkutano wa Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Nchi za Afrika, Karibiani na Pasifiki, unaofanyika Malabo nchini Guinea ya Ikweta. Tarehe 27 Machi 2026. Mazungumzo hayo yamelenga namna ya kukuza na kuimarisha ushirikiano, kuchochea maendeleo na mageuzi ya Jumuiya ya Nchi za Afrika, Karibiani na Pasifiki (OACPS) ili kuweza kukabiliana na changamoto na mahitaji ya sasa. Mazungumzo hayo yamehudhuriwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. James Milya, Balozi wa Tanzania Guinea ya Ikweta mwenye makazi yake Jamhuri ya Kidemokrasia Kongo Mhe. Said Juma Mshana pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Ubelgiji na Umoja wa Ulaya Mhe. Jestas Nyamanga.