Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa katika Matukio tofauti ya picha alipoongoza Watanzania kuaga mwili wa aliyekuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu) na Mbunge wa Jimbo la Isimani, Marehemu Mhe. William Lukuvi katika Viwanja vya Karimjee Jijini Dar es salaam leo Machi 28, 2026.
Mhe. Lukuvi alifariki Dunia tarehe 25 Machi 2026 alipokuwa akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Bejamin Mkapa Mkoani Dodoma.

















