Na Mwandishi wetu Jovina Massano.
Baadhi ya wafanyabiashara na wananchi waiomba tume ya ushindani (FCC) kuendelea kuthibiti na kutoa elimu ili kuepuka athari za matumizi ya bidhaa bandia.
Hayo yamesemwa na wafanyabiashara wa soko kuu la Manispaa ya Musoma mara baada ya kufikiwa na maafisa wa Tume ya ushindani kupata elimu ya bidhaa bandia,mikataba ya mlaji (mikopo inayotolewa na taasisi za fedha)inayotoa vigezo na masharti vilivyoandaliwa na upande mmoja.
Maafisa hao wa ukaguzi bidhaa bandia Mgasi Kalindimya na Thomas Maisory wamewaelimisha wafanyabiashara hao umuhimu wa kutambua bidhaa wanapofanya manunuzi au kuuza bidhaa zao kwa mtumiaji wa mwisho sambamba na vigezo na masharti ya mikopo kwa mlaji (mkopaji).
Tume ya ushindani (FCC) inaendelea kutoa elimu kwa wafanyabiashara mkoani hapa kuondokana na uuzaji wa bidhaa bandia zinazopelekea kuathiri afya kwa walaji.
Akiongea na GMTV Jane Maginga mfanyabiashara wa soko kuu la Musoma mkazi wa Mwisenge amesema hivi sasa bidhaa bandia ni nyingi sana hivyo ni vema FCC kuongeza nguvu katika ukaguaji na uthibiti wa bidhaa ili kupunguza maradhi kwa watumiaji.
"Siku hizi bidhaa bandia ni nyingi sana kwenye madawa,vifaa vya kusafishia kinywa,vipodozi na chakula maradhi yanaongezeka chanzo chake ni bidhaa bandia serikali isimamie kuziondoa bila upendeleo kuokoa wananchi,kansa na kuharibika kwa figo zimeongezeka kwa wingi siku hizi", amesema Jane.
Ameongeza kuwa kwa kiasi kikubwa watu hununua na kutumia bidhaa bila kujua kama itakuathiri kwa kawaida wengi tabia kuchunguza afya mara kwa mara haipo ukaguzi bidhaa uwe wa mara kwa mara kulinda afya za walaji.
Watu wamekuwa wakipata mzio kwa kutumia bidhaa bandia pasipo kujua inakupa changamoto ya Afya.
Kutokana na changamoto hizo Mgasi hakusita kuwaelimisha kwa kuzitaja haki za mtumiaji kuwa ni pamoja na upataji wa mahitaji muhimu,usalama,kuelimishwa,kusikilizwa,kuchagua,kupatiwa taarifa,kutatuliwa malalamiko sanjari na haki ya mazingira mazuri na endelevu ambapo tume ya ushindani (FCC) inazingatia kwa mtumiaji.
Nae Thomas Maisory afisa ukaguzi bidhaa bandia amemalizia kwa kuwakumbusha wajibu wa mtumiaji kwa kuwa makini kuuliza maswali kuhusiana na bei na ubora wa bidhaa na huduma ili kutendewa haki katika kununua huduma,pia kutumia huduma inayostahili kwa kuzingatia athari zinazotokana na mfumo matumizi ya bidhaa na huduma,kusoma maelekezo na kuchukua tahadhari na kuwezakuzingatia usalama wake pindi anapotumia bidhaa na huduma.
Sambamba na hayo pia mtumiaji ana wajibu wa kufuata na kutumia taarifa kabla ya kufanya manunuzi ili kuhakikisha anapata taarifa kamili ya bidhaa au huduma husika.
Lakini pia wajibu wa kupigania na kuzingatia ubora wa bidhaa kupitia utaratibu thabiti wa uwasilishaji wa malalamiko na kutoridhia kununua bidhaa hafifu sanjari na kupunguza uharibifu wa mazingira kwa kuwa makini katika kuchagua na kutumia huduma na bidhaa hii inahusisha uchukuaji hatua za kupunguza taka na kubadili matumizi ya taka pale inapowezekana.





