_▪️Azindua miradi miwili ya Maji ya Ziba hadi Nkinga na Makomero hadi Mgongoro._ _▪️Amtaka Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya Igunga kutenga fedha za ujenzi wa Zahanati._ _▪️Aagiza kuangaliwa upya utaratibu wa utoaji wa vibanda vya wafanyabiashara kwenye halmashauri hiyo._ WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amesema kuwa Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ni kiongozi imara ambaye amedhamiria kuwahudumia Watanzania kwa kuhakikisha huduma za kijamii zinawafikia katika maeneo yao. Amesema hayo kwa nyakati tofauti wakati alipoweka mawe ya msingi ya Miradi ya Upanuzi wa Mtandao wa Majisafi ya Ziwa Victoria kutoka Ziba hadi Nkinga na Makomero hadi Mgongoro, wilayani Igunga mkoani Tabora, Machi 12, 2025. Akizungumza baada ya kuweka jiwe la msingi la mradi wa Ziba hadi Nkinga unaogharimu shilingi bilioni 2.49 na kutarajia kuhudumia wananchi 32,979, Mheshimiwa Majaliwa amesema kuwa Serikali inaendelea kusimamia utoaji wa huduma za maji safi na salama nchini ili kuhakikisha huduma hiyo ina...
Marato tv - Sauti ya Jamii