Na Shomari Binda-Musoma WANAWAKE viongozi na wale wajasiliamali wametakiwa kujiamini wanapokuwa wanatekeleza majukumu yao ya kila siku. Kauli hiyo imetolewa na Naibu Meya wa manispaa ya Musoma Naima Minga alipo zungumza na GMTV leo machi 7 /2025 kuelekea siku ya Wanawake Duniani. Amesema kujiamini ni siraha kubwa kwa mwanamke kutimiza majukumu yake anapokuwa kwenye nafasi ya uongozi au ujasiliamali. Naima amesema kabla ya kuomba nafasi ya kugombea udiwani viti maalum kulikuwa na maneno ya kukatisha tamaa lakini kwa kujiamini kwake kulimfanya kugombea na kushinda. Amesema mwanamke asikubali kukatishwa tamaa na pale anapopata nafasi ya uongozi ni kujiamini pale anapokuwa anatimiza majukumu yae Naibu Meya huyo amesema kuelekea uchaguzi mkuu hapo mwezi oktoba mwaka huu Wanawake wanapaswa kujiamini na kugombea nafasi za uwakilishi wa wananchi ikiwemo udiwani na ubunge. " Kuelekea siku ya wanawake duniani machi 8 nitoe ushauri wangu kwa kila mwanamke kiongozi kujiamini kwenye naf...
Marato tv - Sauti ya Jamii