Skip to main content

Posts

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Waziri Mkuu Asema Hakuna Kusimamisha Zoezi la Uokoaji

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Novemba 18, 2024 amekagua muendelezo wa zoezi la uokoaji katika jengo lililodondoka eneo la Kariakoo Jijini Dar es salaam na amesisitiza kuwa zoezi hilo ni endelevu hadi atakapotolewa mtu wa mwisho aliyekwama kwenye jengo hilo. Aidha Mheshimiwa Majaliwa amelitaka Jeshi la Polisi kuhakikisha wanamtafuta mmiliki wa jengo hilo ili aweze kusaidia kufahamu juu ya chanzo cha kudondoka kwa jengo hilo. Pia ametoa wito wa watanzania kuacha kuchangisha Watanzania kwani Serikali inaoutaratibu wa utoaji wa misaada kupitia Kamati ya Maafa iliyo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu.

Naibu Waziri Mkuu akagua Miradi ya Csr Msimbati Mkoani Mtwara

  *📌 Ahoji matumizi ya Shilingi milioni 159 nje ya bajeti Ujenzi wa Kituo cha Afya Msimbati* *📌 Mkurugenzi wa Halmashauri na Wataamu watofautiana Majibu* *📌 Aiagiza TAKUKURU Kufanya Uchunguzi Ujenzi wa Kituo cha Afya*   *Na Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati* Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko leo Novemba 17, 2024 amefanya ziara Wilayani Mtwara na kukagua ujenzi wa miradi inayotekelezwa kwa fedha zinazotolewa na wawekezaji mbalimbali kwa ajili ya kuboresha maendeleo kama njia ya kurejesha rasilimali kwa wananchi kupitia (CSR). Akikagua Kiktuo cha Afya Msimbati, Dkt. Biteko ameeleza kutoridhishwa na matumizi ya fedha iliyokuwa imepangwa kutumika katika ujenzi wa kituo hicho na kupelekea ongezeko la kiasi cha shilingi milioni 159. Kituo hicho cha Afya awali kilikadiriwa kujengwa kwa gharama ya shilingi milioni 600 lakini gharama za ujenzi huo ziliongezeka hadi kufikia shilingi milioni 759 na hivyo kuibua maswali ambayo Mkurugenzi wa Hal...

Uokoaji Kariakoo ni Ushuhuda wa Moyo wa Watanzania:Nchimbi

_Apongeza wananchi wa kawaida  kwa kujitokeza haraka kuokoa watu_ _Serikali, vyombo vyake na taasisi binafsi zapewa heko kwa mwitikio wa mfano_ KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi, amepongeza utayari na mshikamano ulioonyeshwa na Watanzania mara baada ya tukio la kuanguka kwa jengo Kariakoo, akisema kuwa hatua hizo zimeonesha uzalendo na moyo wa udugu uliojengwa ndani ya Taifa letu. Akizungumza leo, tarehe 17 Novemba 2024, alipotembelea eneo la tukio, Balozi Nchimbi alitoa pole kwa familia za waliopoteza maisha na kuwapa faraja waliojeruhiwa, huku akisisitiza umuhimu wa mshikamano katika nyakati za dharura. “Kwa namna ya pekee, napenda kutoa pole zangu za dhati kwa familia za wenzetu waliopoteza maisha. Maisha ya kila Mtanzania yana thamani kubwa. Tunaomba Mwenyezi Mungu azilaze roho za marehemu mahali pema peponi,” alisema Balozi Nchimbi. Aidha, aliwafariji majeruhi akisema:,’Kwa walioumia, walioko hospitali na hata waliotoka, tunawaombea up...

Mhe.Mchengerwa:Rufaa 5,589 za Wagombea Zimekubaliwa

 WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Mohamed Mchengerwa amesema kati ya rufaa 16,309 za wagombea wa nafasi mbalimbali kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa zilipokelewa, rufaa 5,589 zimekubaliwa. Katika mkutano wake na waandishi wa habari jijini Dodoma leo Novemba 16, 2024, Waziri Mchengerwa amesema rufaa hizo ni pamoja na zilizowasilishwa baada ya muda wa nyongeza wa siku mbili na uamuzi wake umezingatia dosari ambazo zilisababisha kutoteuliwa kwao awali hazikuwa kubwa zinazoathiri matokeo yaliyokusudiwa na kanuni.  Aidha, amesema katika nafasi zinazogombewa vyama 18 vya siasa vimeweka wagombea katika nafasi 30,977 kati ya nafasi 80,430 sawa na asilimia 38.51 huku Chama cha Mapinduzi (CCM) kikiweka wagombea katika nafasi zote.  Amesema katika nafasi za mwenyekiti wa kijiji zinazogombewa ni 12,280 ambapo vyama hivyo vimeweka wagombea katika nafasi 6,060 sawa na asilimia 49.35. Pia, amesema nafasi za mwenyekiti wa mtaa zinazogombewa ni...

Juliana Masaburi aomba Mifuko ya Mikopo iwafikie Vijana Wote

MBUNGE wa viti maalum kupitia vijana mkoa wa Mara Mhe. Juliana Didas Masaburi amesema Ofisi ya Waziri Mkuu ina Mifuko zaidi ya 71 yenye fursa za kuwawezesha vijana lakini haiwafikii walengwa katika kuondoa tatizo kwa ajira kwa kundi hilo kubwa nchini. Mh Masabari ametoa rai hiyo kwenye kongamano aliloliitisha kwa ajili kuangalia fursa  za kiuchumi kwa vijana wa mkoa wa Mara na kufanyika ukumbi wa CMG mjini Tarime Amewaambia Vijana zaidi ya 1,000 kutoka Wilaya zote Saba za Mkoa wa Mara na Mikoa ya jirani kuwa endapo mifuko hiyo kutoka ofisi ya waziri mkuu ingetumika kikamilifu ingweza kusaidia mitaji kwa vijana na hivyo kupunguza tatizo la ajira nchini. Katika kongamano hilo vijana walipata mafunzo kutoka kwa Wakufunzi na Wataalam wa Wizara ya Madini, Wizara ya Nishati, Wizara ya TAMISEMI, Ofisi ya Waziri Mkuu na Taasisi kadhaa "Tutakuwa viongozi waongo tukiwaambia kuwa Serikali ya CCM au Serikali ya Awamu ya Sita itawaletea fedha mifukoni mwenu vijana kila siku au kila mwisho wa m...

Dkt.Biteko awataka Wahitimu Wasiogope Changamoto za Maisha baada ya Chuo

 *📌 Awahimiza kufanya uamuzi sahihi, kujibu maswali na dukuduku walizonazo* *📌 Apongeza ushirikiano wa Serikali na Sekta Binafsi katika maendeleo nchini* *📌 SAUT yamshukuru Rais Dkt. Samia kwa miongozo katika sekta ya elimu* *Na Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati* Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amewahimiza wahitimu katika ngazi mbalimbali kutumia taaluma yao kufanya maamuzi sahihi yatakayowawezesha kupata majibu ya maswali na dukuduku walizonazo kuelekea maisha mapya. Dkt. Biteko ametoa rai hiyo Novemba 16, 2024 katika Mahafali ya 13 ya Chuo Kikuu Kishiriki, Stella Maris cha Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino, Mtwara.  Pamoja na kuwapongeza wahitimu kwa kuhitimu amewataka kutumia taaluma waliyoipata kuwa nyenzo katika utatuzi wa changamoto watakazokabiliana nazo maishani baada ya kuondokana na maisha ya chuo.  “ Wengine wanaendelea kujiuliza, nini kitafuata baada ya kuhitimu? Uelekeo utakuwa ni upi? na wengine wanasema hali s...