Na Mwanamkuu Mwandoro,Tanga
TAASISI za serikali zinazotengeneza magari yake nje ya mfumo wa Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania (TEMESA) zimetakiwa kuacha mara moja tabia hiyo kwani inasababisha upotevu mkubwa wa fedha kwa serikali .
Akizungumza changamoto hiyo Meneja wa TEMESA Mkoa wa Tanga Mhandisi Riziki Lukali amesema y magari ya serikali yaliyosajoliwa kwaajili ya kufanyiwa matengenezo TEMESA ni zaidi ya 200 lakini yanayo kwenda kwao ni machache mno.
Aidha Mhandisi Lukali ameongeza kuwa ili kutatua changamoto hiyo anahitaji kuonana na taasisi zote za serikali zinazofanya hivyo ili kujua changamoto ni nini na kutafuta suluhisho la kudumu.
Sambamba na hayo Mhandisi Lukali pia ametoa onyo kali kwa gereji zote zilizopatiwa kibali cha kutengeneza magari ya serikali na badala yake kutumia vibaya vibali hivyo kwa kupokea magari bila kuwa na kibali cha gari husika.
"Najua kuwa kuna gereji zinazotumia vibaya nafasi walipewa ya kupatiwa vibali vya kutengeneza magari ya serikali kwa kupokea magari hayo kinyume cha sheria kwani wanajua kuwa hawapaswi kupokea gari kwaajili ya matengenezo ambalo halina kibali husika kutoka TEMESA,na wapo pia wanaogushi vibali hivyo,atakaye bainika kufanya hivyo hatutamuacha salama", amesema Mhandisi Lukali.
Mhandisi Lukali pia ametoa wito kwa viongozi wa taasisi za serikali wanaoangalia unafuu wa gharama za matengenezo bila kujali ubora wa Huduma wanazokwenda kupatiwa huko wanapokwenda kinyemela na kuwaacha TEMESA ambao kwa sasa wana mafundi wazuri,vifaa bora na vya kutosha pamoja na matumizi ya teknolojia ya kisasa.Mpaka sasa kwa Tanga gereji zilipewa vibali kutoka TEMESA vya kutengeneza magari ya serikali ni tatu,ambazo ni Lal garage, Adams motor na Toyota,hata hivyo TEMESA hawayosita kufata kibali hicho kwa atakaye bainika kufanya kazi kinyume na makubaliano.

Comments
Post a Comment