Na Mwandishi wetu Jovina Massano Musoma.
Vijana watakiwa kujitambua na kuchangamkia fursa ziletwazo na serikali waondokane na malalamiko ya ukosefu wa ajira.
Hayo yamesemwa katika Kongamano la Kimataifa la kumi na moja la Kilimo misitu lililozinduliwa Oktoba 19,2026 na Katibu Tawala wa mkoa wa Mara katika viwanja vya Kituo Cha mafunzo ya kilimomisitu kilichopo Kata ya Bweri Manispaa ya Musoma mkoani Mara.
Kila Mwaka Vi Agroforestry huandaa kongamano la Kilimo kwa lengo kuhamasisha uwekezaji,kuimarisha ushirikiano na kuchochea utekelezaji wa mkakati wa kilimomisitu nchini.
George Kamongo na Mzee Christopher wakazi wa Bukabwa wilayani Butiama wamesema Serikali inawajali Sana Vijana lakini wao ndio hawako tayari kuchuchangamkia fursa zinaziletwa na serikali na wadau mbalimbali wa maendeleo.
Wamesema kuwa kuna haja ya vijana kujitambua kuwa tayari kupata elimu na makongamano yanayoandaliwa na serikali wawe na mwitikio ili kupata fursa mbalimbali.
" Tunaomba Vijana wajitambue wawe na mwitikio fursa hii ni adimu hapa kwa kiasi kikubwa wazee ndio wengi,sisi tunaishukuru serikali kuweza kuwakumbuka na wao waone serikali yao inawapenda wafike ili wajifunze na washiriki kupata elimu ya uwekezaji na kilimomisitu", amesema mzee Christopher.
Wamesema Vijana hawana mwitikio wa fursa muhimu zinazoletwa na taasisi mbalimbali hasa zenye kuwaletea manufaa katika safari ya maisha na kuwainua kiuchumi zinazochochea na kuwaletea maendeleo.
"Fursa zinaletwa mwitikio hafifu matokeo yake madai ya ukosefu wa ajira na madai ya kupatiwa haki ndio yanasikika ni vema wakawa wawajibikaji badala ya malalamiko", amesema George.
Martha Olutu Meneja mkazi wa Vi Agroforestry Tanzania amesema kongamano hili linalenga kubadili fursa za kilimomisitu kuwa uwekezaji pia lunatarajia kuwakutanisha takribani washiriki 8,000 ana kwa ana na kwa njia ya mtandao.
" Kongamano hili limelenga fursa za kilimomisitu kuwa uwekezaji unaotekelezeka,utakaichochea fursa za uchumi kwa vijana ikiwemo kuimarisha usalama wa chakula na kuchangia urejeshaji wa mandhari ukijumuisha ardhi, misitu,vyanzo vya maji na mifumo ya ikologia", amesema Martha.
Katika Kongamano litakuwa na mdahalo utawakutanisha Vijana na watunga sera, taasisi za fedha wawekezaji, wakulima,na wafanyabiashara ili kujadili vikwazo vinavyowakabili katika kupata mitaji,ardhi,masoko na huduma za kitaalam.
Kwa Upande wake Mgeni rasmi Gerald Musabila Kusaya amewahamasisha wananchi wote wakiwemo vijana kushiriki katika Kongamano ili waweze kujifunza fursa mbalimbali zilizopo katika kilimomisitu kuboresha maisha.
Hakusita kutoa shukrani kwa Shirika la Vi Agroforestry na washirika wake kwa kuwa wananchi wanapata fursa ya kujifunza teknolojia na bunifu mbalimbali za kilimomisitu.
Vi Agroforestry ni shirika la Kimataifa la Maendeleo kutoka Sweden lenye lengo la kupunguza umaskini na kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi kupitia kilimomisitu na usimamizi endelevu wa ardhi ya kilimo pia hushirikiana na familia za wakulima wadogo kuendeleza mifumo endelevu ya uzalishaji lilianzishwa Mwaka 1983.









Comments
Post a Comment