Na Mwandishi wetu Jovina Massano.
Mkoa Kigoma umekuwa ukipokea wakimbizi wengi kwa miaka mingi kumekuwa na utumiaji mwingi wa nishati ya kuni hali iliyopelekea uharibifu wa mazingira.
Mara baada ya kupata maelezo mafupi katika banda la Vi Agroforestry kutoka kwa Afisa ufuatiliaji na tathmini Stella Msami kuwa hivi sasa kuna mradi wa miaka mitatu utakaopelekea vijana wengi kujifunza hivyo amemtaka mgeni rasmi kupendekeza mkoa ambao utakuwa ni mmojawapo wa wanufaika wa mradi huo.
Amesema Stella kutokana na uwepo wa mradi huo wa kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi tutajitahidi kufikisha ujumbe wa upandaji miti kwa mkoa pendekezwa ukizingatia kwamba upandaji miti ndio nguzo pekee itakayosaidia kukabili mabadiliko ya tabia nchi.
Kwa Upande wake Katibu Tawala mkoa wa Mara Gerald Musabila Kusaya amelitaka shirika la Vi Agroforestry kuongeza juhudi za upandaji miti Mkoa wa Kigoma kutokana na uwepo wa historia ya matumizi makubwa kuni.
" Tunakwenda kupanda miti kule Kigoma kwa sababu kwa historia ukifuatilia ni mkoa ambao umekuwa ukipokea wakimbizi kwa wingi na wanapokuja nishati kubwa wanayotumia ni kuni kwa hiyo ukataji wa miti ni mkubwa mno ndio maana nimependekeza huko ili miti iliyokatwa na wakimbizi maeneo yaliyoathirika yarudi katika hali yake", amesema Kusaya.
Stella ameongeza kuwa kuna umuhimu mkubwa wa kushirikisha jamii hasa Vijana kwa sababu fursa nyingi bado hazijatumika kuanzia kwenye uzalishaji hadi kwenye masoko.
"Kuna fursa ya upandaji miti kwa kutengeneza vitalu na kuuza pia Kuna fursa za kuchakata mazao yanayotokana na kilimomisitu na kujipatia kipato na kujiendeleza na kujipatia ajira", amesema Stella.
Katika maonyesho haya kuna Banda la maarifa ambalo Vijana wanakutanishwa na wataalamu mbalimbali kutoka vyuo vikuu waliofanya tafiti na wakajua fursa zilizopo na rafiki kwa vijana na wanatakiwa kufika na kupata maarifa kuanzia kwenye kuzalisha hadi kwa mraji wa mwisho.
Pia amezisisitiza uwepo wa sera rafiki kwa vijana itakayoweza kusaidia Vijana kutumia fursa zilizopo kwa kuweka utaratibu wa upatikanaji wa ardhi,mitaji na teknolojia kwa urahisi na hii itahitaji ushirikiano wa wabia wa maendeleo kuwasaidia vijana hapa nchini.
Hata hivyo Katibu Tawala amepata fursa ya kupanda mti wa mfano katika ramani ya Tanzania na kutembelea vipando na mabanda yenye bidhaa zitokanazo na kilimomisitu kwa maendeleo endelevu.









Comments
Post a Comment